Operesheni Panama

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Operesheni Panama ni riwaya ya kipelelezi ilioandikwa na Japhet Nyang'oro Sudi na kutoka mwaka 2019 [1] Ni riwaya inayozungumzia sana utakatishaji fedha unavyofanyika na jinsi fedha hizo zinavyoweza kutoroshwa katika nchi husika, zikaenda nchi nyingine na baadaye kurejea tena katika nchi ya kwanza na kuonekana ni fedha halali.

Katika riwaya hii mhusika mkuu Mike Dagas anarejea nchini akitoka katika mafunzo ya ujasusi aliyyachukua kwa takribani miaka zaidi ya kumi, lakini kabla hata ya kufika nyumbani kwake anajikuta akiaanza kufuatiliwa na jasusi mmoja mbobezi na mtunza siri mkuu wa jeshi aitwaye mtaalamu wa fundi na kupewa kazi nzito ya kufuatilia watakatishaji wa fedha. Safari ya kufuatilia watakatisha fedha inaanza katika mazingira magumu ambayo Mike Dagas analazimika kuwa kichaa ili kufahamu mengi yaliyopo katika biashara hiyo.

Mwisho, Mike Dagas anajikuta akifika nchini Panama na kufanikiwa kukomboa kiasi kikubwa cha fedha lakini ikiwa tayari maisha ya watu wengi yamepotea.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Sudi, Japhet Nyang'oro, 1981-. Operesheni Panama. [Dar es Salaam]. ISBN 978-9987-794-05-8. OCLC 1073034179. 
Makala hii kuhusu kitabu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Operesheni Panama kama Mwandishi wake, hadithi au matoleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.