Nenda kwa yaliyomo

Nyumba ya Mambo Msiige

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nyumba ya Mambo Msiige ikionekana kwa mbali.

Nyumba ya Mambo Msiige ni jengo la kihistoria kwenye ufukwe wa Shangani, Mji Mkongwe Zanzibar. Lilijengwa mnamo 1850 na tajiri mkazi wa Kiarabu, Salum bin Harith.[1][2]

Jengo hilo lilitumika kama makazi ya wawakilishi wa Waingereza, misheni ya Vyuo Vikuu katika Afrika ya kati na hospitali ya Uropa.[2]

Usanifu wa jengo lenyewe umejumuisha mchanganyiko wa kuvutia wa ushawishi wa Waswahili, Waajemi pamoja na matao ya mtindo wa Omani na uchoraji wa mbao.[3]

  1. http://fahariyazanzibar.blogspot.com/2010/01/mambo-msiige.html
  2. 2.0 2.1 "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-05-12. Iliwekwa mnamo 2021-05-10.
  3. https://www.expertafrica.com/zanzibar/stone-town/park-hyatt/in-detail