Nyuki-kekeo
Nyuki-kekeo | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Coelioxys froggatti
| ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
| ||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||
Familia 3 zenye nyuki-kekeo na jenasi 8 katika Afrika ya Mashariki:
|
Nyuki-kekeo (kutoka kwa Kiing. cuckoo bees) ni nyuki waliotaga mayai yao katika viota vya nyuki wengine, kama vile kekeo hufanyia ndege wengine. Kuna makundi mbalimbali ya nyuki-kekeo. Jenasi iliyoenea zaidi na kuwa na spishi nyingi barani Afrika ni Coelioxys ya familia Megachilidae yenye spishi 21 katika Afrika ya Mashariki. Jenasi nyingine ya familia hii, Euaspis, ina spishi chache, ambazo moja tu imerekodiwa kutoka Afrika ya Mashariki. Makundi mengine hutokea katika familia Apidae, muhimu zaidi duniani kote ikiwa nusufamilia Nomadinae yenye spishi 14 katika Afrika ya Mashariki. Kabila Melectini ina spishi 20 za Afrika ya Mashariki katika jenasi Afromelecta na Thyreus. Makabila mengine nne zilizo na nyuki-kekeo hazipatikani Afrika (Bombini, Ericrocidini, Euglossini na Isepeolini). Katika familia Halictidae jenasi Sphecodes ina spishi 6 za nyuki-kekeo katika Afrika ya Mashariki.
Maelezo
[hariri | hariri chanzo]Kwa sababu nyuki hawa wako katika makundi mbalimbali ya kitaksonomia, haiwezekani kutoa maelezo ya wao wote pamoja. Tembelea kurasa maalum kwa taarifa zaidi. Hata hivyo, kwa ujumla, nyuki hawa hawachomi au mchomo wao sio chungu hasa. Pia huwa na kutikulo ngumu kuhimili mashambulizi ya mdusiwa wao. Kwa sababu hiyo hiyo, wanaweza kuwa na marekebisho mengine.
Kama jina lao linavyoonyesha, nyuki hawa wana tabia kama kekeo kwa maana kwamba wao pia hawajengi viota vyao wenyewe, lakini hutaga mayai kwenye viota vya nyuki wengine, kwa kawaida wapweke. Nyuki mdusiwa wanaweza hata kuwa katika kundi moja la kitaksonomia na wanaweza kuwa na uhusiano wa karibu. Spishi nyingine hudusia nyuki wasiohusiana, pengine spishi mdusiwa moja tu au vinginevyo spishi kadhaa.
Spishi za Afrika ya Mashariki
[hariri | hariri chanzo]
Apidae
|
Halictidae
Megachilidae
|
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Afromelecta lieftincki
-
Thyreus histrionicus
-
Epeolus bifasciatus
-
Pasites maculatus
-
Sphecodes albilabris
-
Coelioxys octodentata