Nenda kwa yaliyomo

Nyoka Mchimbaji

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nyoka mchimbaji
Nyoka mchimaji wa Israel (Atractaspis engaddensis)
Nyoka mchimaji wa Israel (Atractaspis engaddensis)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Reptilia (Wanyama wenye damu baridi na magamba ngozini)
Oda: Squamata (Mijusi, mijusi-nyungunyungu na nyoka)
Nusuoda: Serpentes (Nyoka)
Familia: Lamprophiidae (Nyoka walio na mnasaba na chata)
Fitzinger, 1843
Nusufamilia: Atractaspidinae (Nyoka wanaofanana na nyoka wachimbaji)
Günther, 1858
Jenasi: Atractaspis
A.Smith, 1849
Ngazi za chini

Spishi 22:

Nyoka wachimbaji ni nyoka wenye sumu wa jenasi Atractaspis katika familia Lamprophiidae. Wana jina hili kwa sababu huchimba ardhini.

Nyoka hawa ni wafupi na wembamba lakini spishi kadhaa zinaweza kuwa nene kiasi. Urefu wao ni sm 30-70 na m moja kwa kipeo. Rangi yao ni nyeusi, kijivu au kahawia. Spishi mbili kutoka Pembe ya Afrika, nyoka mchimbaji wa Ogadeni na nyoka mchimbaji Somali, zina mabaka meupe kichwani au kichwa kizima ni cheupe.

Nyoka wachimbaji huishi katika vishimo au katika udongo au mchanga tebwere. Hula mijusi wenye ngozi nyororo, amfibia na nyoka wadogo, na hukamata wagugunaji katika vishimo vyao.

Chonge ni meno ya mbele. Nyoka hafungui mdomo lakini anavuta kidevu nyuma na kuzungusha chonge kuelekea mbele na kupota kichwa kitongo, chini na nyuma ili kudunga mhanga. Anaweza kufanya hii hata akishikwa kwa kichwa na mtu, kwa hivyo hata wataalamu wa nyoka wanaweza kudungwa. Hatari ni kama nyoka hawa wanafanana na nyoka wengine wasiodhuru. Kwa bahati nzuri sumu ya nyoka hawa siyo hatari sana isipokuwa ile ya nyoka wakubwa wa spishi kadhaa kama nyoka mchimbaji kijivu.

Spishi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Spawls, S., Howell, K., Drewes, R. & Ashe, J. (2002) A field guide to the Reptiles of East Africa. Academic Press, San Diego, CA, USA.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nyoka Mchimbaji kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.