Nyoka-maji (Grayia)
Mandhari
Nyoka-maji | ||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
| ||||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||||
Spishi 4:
|
Nyoka-maji wa jenasi Grayia ni nyoka wasio na sumu katika familia Lamprophiidae. Kuna nyoka-maji katika jenasi Lycodonomorphus wa familia hiyo hiyo pia, lakini nyoka hawa ni wafupi zaidi kwa kima cha 50%.
Nyoka hawa ni warefu kiasi. Spishi kubwa inaweza kufika m 2.5 lakini urefu wa wastani ni sm 70-150. Wana mkia mrefu (hadi 40% ya urefu wa jumla). Rangi yao ni hudhurungi hadi nyeusi na kuna mabaka meupe au kijivu mbavuni.
Spishi za Grayia huishi majini katika misitu ya mvua ya Afrika ya Kati na spishi mbili zinatokea Afrika ya Mashariki pia. Hula vyura na samaki wadogo.
Nyoka hawa hawana sumu na kwa hivyo wanaweza kukamatwa bila hatari licha ya urefu wao.
Spishi
[hariri | hariri chanzo]- Grayia caesar, Nyoka-maji wa Caesar (Caesar's African water snake)
- Grayia ornatus, Nyoka-maji Maridadi (Ornate African water snake)
- Grayia smythii, Nyoka-maji wa Smyth (Smyth's African water snake)
- Grayia tholloni, Nyoka-maji wa Thollon (Thollon's African snake)
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Spawls, S., Howell, K., Drewes, R. & Ashe, J. (2002) A field guide to the Reptiles of East Africa. Academic Press, San Diego, CA, USA.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Nyoka-maji (Grayia) kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |