Nyoka-maji
Nyoka-maji | ||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Nyoka-maji kahawia (Lycodonomorphus rufulus)
| ||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
| ||||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||||
Spishi 9:
|
Nyoka-maji ni nyoka wasio na sumu wa jenasi Lycodonomorphus katika familia Lamprophiidae. Kuna nyoka-maji katika jenasi Grayia wa familia hiyo hiyo pia, lakini nyoka hawa ni warefu zaidi mara mbili. Na pia tena kuna nyoka-maji katika familia Colubridae.
Spishi hizi ni fupi kiasi, sm 70 kwa kipeo lakini sm 35-60 kwa kawaida. zina mkia mfupi, kichwa kidogo na macho madogo. Rangi yao ni nyeusi, kijivu, kahawia, hudhurungi, kahawia-zeituni au kijani-zeituni juu na mara nyingi njano au machungwa chini.
Nyoka-maji huishi majini na hula vyura na samaki wadogo.
Nyoka hawa hawana sumu na kwa hivyo wanaweza kukamatwa bila hatari.
Nyoka-nyumbani
[hariri | hariri chanzo]Spishi moja, nyoka-nyumbani mweusi (Lycodonomorphus inornatus) ni tofauti na spishi nyingine za jenasi hii. Haiishi majini na inaweza kuingia nyumba. Hula mijusi, nyoka wengine na wagugunaji wadogo. Nyoka huyu ni mrefu kuliko wenzake, hadi sm 130.
Spishi
[hariri | hariri chanzo]- Lycodonomorphus bicolor, Nyoka-maji wa Ziwa Tanganyika (Lake Tanganyika water snake)
- Lyocodonomorphus inornatus, Nyoka-nyumbani Mweusi (Black house snake)
- Lycodonomorphus laevissimus, Nyoka-maji Tumbo-kijivu (Dusky-bellied water snake)
- Lycodonomorphus leleupi, Nyoka-maji Tumbo-jeusi (Black-bellied water snake)
- Lycodonomorphus mlanjensis, Nyoka-maji wa Mlanje (Mlanje water snake)
- Lycodonomorphus obscuriventris, Nyoka-maji wa Msumbiji (Floodplain water snake)
- Lycodonomorphus rufulus, Nyoka-maji Kahawia (Brown water snake)
- Lycodonomorphus subtaeniatus, Nyoka-maji wa Kongo (Congo white-bellied water snake)
- Lycodonomorphus whytii, Nyoka-maji wa Whyte (Whyte's water snake)
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Nyoka-nyumbani mweusi
-
Nyoka-maji kahawia
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Spawls, S., Howell, K., Drewes, R. & Ashe, J. (2002) A field guide to the Reptiles of East Africa. Academic Press, San Diego, CA, USA.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Nyoka-maji kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |