Nje ya Bongo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nje ya Bongo
Nje ya Bongo Cover
Studio album ya Mr. II
Imetolewa 1999
Imerekodiwa 1998-99
Aina Bongo Flava, Hip hop
Lebo Greenfields Forever Studio
Mtayarishaji Mongo Star
II Proud
Wendo wa albamu za Mr. II
"Niite Mr. II"
(1998)
"Nje ya Bongo"
(1999)
"Milenia"
(1999)

Nje ya Bongo, ni jina la albamu ya nne kutoka kwa msanii wa muziki wa hip hop wa Dar es Salaam, Tanzania maarufu kama II Proud. Albamu imetoka mwaka 1999, mwaka mmoja tangu atoe albamu ya tatu. Nyimbo kali kutoka katika albamu ni pamoja na Deiwaka, Nje ya Bongo, Nipo Kwenye Microphone na Siku Yangu. [1] Albamu imefanywa kipindi ambacho 2 Proud ndiyo mara yake ya kwanza kufanya safari ya Ulaya na kurekodi nyimbo hizo akiwa hukohuko barani Ulaya.

Albamu imetayarishwa na Mongo Star amemtaja katika wimbo wa Nje ya Bongo, vilevile II Proud nae katia mkono katika kutayarisha albamu hii. Kifupi hakuna albamu ambayo 2 Proud hajashiriki katika kutayarishaji kasoro Coming of Age-Ujio wa Umri tu. Zilizobakia zote katia mikono yake. DJ Jumanne alisaidia katika kutayarisha albamu hii.[2] Halafu kipindi hiki si zamani sana tangu J4 afanye utafiti wake wa muziki wa hip hop wa Tanzania.


Orodha ya nyimbo[hariri | hariri chanzo]

 1. A1 - Deiwaka
 2. A2 - Busara
 3. A3 - Niko Fresh
 4. A4 - Dunia
 5. A5 - Siku Yangu
 6. B1 - Nje Ya Bongo
 7. B2 - Stori
 8. B3 - Ni Ndoto
 9. B4 - Mwanamuziki
 10. B5 - Nipo Kwenye Microphone

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]


Marejeo[hariri | hariri chanzo]

 1. Nje ya Bongo katika wavuti ya Discogs
 2. Nje ya Bongo. Kiswahili rap Keeping it Real (1998) katika wavuti ya African Hip Hop.com. Ingizo la February 23, 2003.