African Hip Hop.com

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nembo ya Africanhiphop.com

Africanhiphop.com ni moja kati ya wavuti mtandaoni inayochochea tamaduni za Kiafrika mijini. Wavuti inamilikiwa na DJ Jumanne ambaye aliizisha mwaka 1997. Awali ilitengenezwa kwa lengo la kuwaleta watu pamoja ambao kwa namna moja au nyingine wamevutiwa na utamaduni wa muziki wa hip hop na wa Afrika kwa ujumla ambao hadi leo hii upo. Africanhiphop.com inatoa taarifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na mahojiano, habari kemkem, DJ mix na redio za mtandaoni. Vilevile ina ukumbi wa majadiliano ambao unaunganisha watu mbalimbali duniani.

Taarifa zinazopatikana katika Africanhiphop.com zinatolewa au kuchangiwa na watu mbalimbali duniani, kuanzia Africa na kwengineko, na wakati mwingine habari hizo huchangiwa na wasanii wenyewe.

Africanhiphop.com inajiendesha yenyewe bila msaada kutoka kwa mtu yeyote. Kwa miaka mingi wamekuwa wakishirikiana na mashirika mbalimbali katika kutekeleza baadhi ya kazi. Mashirika hayo ni pamoja na Madunia Foundation, Africaserver na This Is Africa.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Wavuti ya Africanhiphop.com, zamani ikiitwa Rumba-Kali, ilianzishwa mnamo mwezi Februari 1997 kama jukwaa la taarifa na majadiliano juu ya hip hop kutoka barani Afrika. Wakati huo inaanzishwa kulikuwa hakuna mtandao au wavuti ambayo inachapisha ama kutoa taarifa za muziki wa hip hop barani Afrika. Ukiachailia mbali baadhi ya wasanii wa hip hop kama vile kundi POC kutoka Afrika Kusini, na PBS kutoka Senegal hakuna wengine waliokuwa wanaeneza au kutambulisha harakati za hip hip Afrika nzima. Kwa vile kulikuwa hakuna mawasiliano baina ya wasanii wa Afrika, kwa mfano mawasiliano baina ya Senegal na Afrika Kusini, wavuti ya Rumba-Kali iliingilia kati na kuunganisha mawasiliano hayo.

Miaka ya kwanza ya ufunguzi wa wavuti hii mengi yalitokea. Hip Hop barani Afrika – na duniani kote ililipuka. Makundi ya muziki wa hip hop ya Afrika yalitoa albamu na kuweza kufanya ziara mbalimbali huko Afrika kwenyewe, Japan, Ulaya, Marekani na Australia. Matamasha mbalimbali ya Umajumui wa Afrika yalifanyika. Kuanzia hapo, wavuti ya Rumba-Kali ilianza kuvutia watu wengi zaidi kuitembelea, na kupelekea hata wale watu ambao awali walikuwa hawajui kama Afrika inafanya hip hop nao walionesha upendo. Watu wengi kutoka nchini Marekani na kwingineko duniani walifurahia kuungana na watu wa nyumbani katika harakati. Wengine waliona ni vyema kuungana na asili yetu ambayo kwa sasa imeona njia ya nyumbani kule ilikotoka.

Africanhiphop.com sasa inafanyakazi kama moja kati ya chombo au chanzo kikuu cha taarifa kuhusu muziki wa hip hop wa Afrika. Habari zake nyingi zilipatwa kutumiwa na mitandao mikubwa ya vyombo vya habari vya kimataifa kama vile BBC, BET, Source na wengine wengi. Kwa kusoma taarifa zilizopo katika wavuti hii, watu waliweza kuandaa dokumentari, majarida, vipindi vya elimu na hata filamu huko Hollywood walifaidika na taarifa za Africanhiphop.com. Katika ukumbi wa majadiliano wa umekuwa kituo kikuu cha wakongwe wa muziki wa hip hop wakijadiliana kupeana mawazo mbalimbali – hata kandamseto za Kamajumui wa Afrika zilizaliwa na majadiliano, hata muungano wa wasanii wa Zambia-Nigeria, vilevile hata ndoa ziliunganishwa na majadiliano ya mtandao huu.

Tangu kuanzishwa kwake, kumekuwa na mitandao mingi sana kuhusu hip hop ya Afrika lakini Africanhiphop.com inabaki kuwa mama au mwanzilishi wa ugavi wa taarifa za hip hop ya Afrika.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]