Nenda kwa yaliyomo

Natasha Henstridge

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Natasha Henstridge
Jina la kuzaliwa Natasha T. Henstridge
Alizaliwa 15 Agosti 1974
Kanada
Kazi yake Mwigizaji
Mwanamitindo
Miaka ya kazi 1995 - hadi leo
Ndoa Damian Chapa (1995-1996)

Natasha T. Henstridge (amezaliwa tar. 15 Agosti 1974) ni mwigizaji wa filamu-mwanamitindo kutoka nchini Kanada. Anafahamika zaidi kwa kucheza katika mfululizo wa filamu za Species I na Species II.

Maisha ya awali

[hariri | hariri chanzo]

Henstridge alizaliwa mjini Springdale, Newfoundland na Labrador, Kanada, akiwa kama binti wa Helen, mama wa nyumbani, na Brian Henstridge, mkandarasi wa baiskeli. Natasha alikulia mjini Fort McMurray, Alberta, Kanada akiwa na mdogo wake wa kiume aitwaye Shane.

Akiwa na umri wa miaka kumi na tatu, alijiunga na Casablanca Modeling Agency, ambao wao walikuwa kama wakala wa wanamitindo. Hapo alijiunga kwa lengo la kumtafuta kisura wa mwaka, na kwa bahati nzuri akachuguliwa kuwa mshindi wa kwanza.

Mwaka uliyofuatia, Henstridge alielekea mjini Paris kwa lengo la kukuza kipaji chake cha uwanamitindo. Akiwa na umri wa miaka kumi na tatu, akachapishwa katika ukurasa wa mwanzo wa gazeti la Kifaransa la cosmopolitan.

Akaendelea kutolewa katika kurasa ya mwanzo katika magazeti chungu mzima na baadaye Henstridge akaelekea zake katika mishughuliko ya kiabishara katika televisheni na akafanikiwa kutoka katika Olay, Old Spice, na Lady Stetson. Baada ya kuwa madhubuti katika uwanamitindo, Henstridge akajiingiza katika maswala ya uigizaji wa filamu.

Maisha binafsi

[hariri | hariri chanzo]

Henstridge aliolewa mara mbili na mume mmoja (Damian Chapa). Ingawaje, ndo ya pili iliisha miezi michache tangu kuoana na taraka rasmi ikifuata mnamo mwaka wa 1996. Ana watoto wawili aliozaa na mwigizaji wa filamu Bw. Liam Waite, wa kwanza anaitwa Tristan River Waite, amezaliwa Oktoba 1998, na Asher Sky Waite, amezaliwa mwezi wa Septemba katika mwaka wa 2001. Rafiki yake wa muda mrefu ni miwgizaji, mwimbaji-mtunzi wa nyimbo wa Uskoti Bw. Darius Danesh.

Filamu alizocheza

[hariri | hariri chanzo]
  • Species (1995)
  • Maximum Risk (1996)
  • Adrenalin: Fear the Rush (1996)
  • Bela Donna (1998)
  • Dog Park (1998)
  • Species II (1998)
  • Caracara (1999)
  • The Whole Nine Yards (2000)
  • Second Skin (2000)
  • It Had To Be You (2000)
  • Ghosts of Mars (2001)
  • Kevin of the North (2001)
  • She Spies (2002)
  • Steal (2002)
  • Species III (2004)
  • The Whole Ten Yards (2004)
  • Widow On The Hill (2005)
  • Deception (2008)

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]