Nassor Hamoud

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nassor Saadun Hamoud
Maelezo binafsi
Tarehe ya kuzaliwa 23 Machi 2001
Mahala pa kuzaliwa    Tanzania
Nafasi anayochezea Kiungo wa kati
Timu ya taifa
Timu ya Taifa ya Tanzania

* Magoli alioshinda

Nassor Saadun Hamoud, (alizaliwa tarehe 23 Machi 2001) ni mchezaji wa soka nchini Tanzania, ambaye anachezea klabu ya Šumadija Aranđelovac nchini Serbia.

Klabu[hariri | hariri chanzo]

Katika nchi yake Tanzania Hamoud aliichezea Kagera Sugar katika mashindano ya Ligi Kuu Tanzania Bara.[1] Kuanzia 2018 hadi 2020 aliichezea klabu ya Tersana SC ya Daraja la Pili nchini Misri. Mnamo Februari 2020 alienda Ulaya na kujiunga na klabu ya OFK Žarkovo ya Ligi daraja la kwanza nchini Serbia kwa msimu wa 2019 - 2020 kwa mkataba wa miaka miwili.[2] Kwa jumla, alicheza mechi mbili katika ligi chini ya klabu hiyo na mechi yake ya kwanza ilikua 30 Mei 2020 dhidi ya FK Zlatibor Čajetina.[3] Kisha akahamia klabu ya FK Šumadija Aranđelovac kabla ya kuuuzwa kwa mkopo katika klabu ya MFK Vyškov mnamo 2021.[4]

Ushiriki Kimataifa[hariri | hariri chanzo]

Hamoud aliitwa kwenye kikosi cha Tanzania kilichoshiriki mashindano ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2021 na alionekana katika mechi zote katika mashindno hayo.[4][5]


Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Kagera Sugar Roster. Kagera Sugar FC.
  2. NINJA, NASSORO MOHAMMED WAPATA DILI LA KUKIPIGA ULAYA, WAKWEA PIPA LEO (Swahili). Saleh Jembe.
  3. Prva Liga profile (Serbian). Prva Liga.
  4. 4.0 4.1 Black Satellites To Face Ngorongoro Heroes In Group C. sportsworld2day.com. Jalada kutoka ya awali juu ya 2023-03-12. Iliwekwa mnamo 2023-03-12.
  5. Soccerway profile. Soccerway.
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nassor Hamoud kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.