Nenda kwa yaliyomo

Mzingo antaktiki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mstari wa mzingo antaktiki kwenye ramani ya Dunia.
Mzingo antaktiki kwenye ramani ya Antaktiki.

Mzingo antaktiki (kwa Kiingereza: Antarctic circle) ni mstari wa kudhaniwa kwenye uso wa Dunia kwa latitudo ya kusini ya 66° 33' 50 hivi[1]. Umbali wake na ncha ya kusini ni takriban kilomita 2,600, umbali kutoka ikweta km 15,996.

Kinyume chake ni mzingo aktiki upande wa kaskazini ya Dunia.

Ufafanuzi wa mzingo antaktiki[hariri | hariri chanzo]

Mzingo antaktiki unafafanuliwa na latitudo ambako Jua linaanza kuonekana kwa saa 24 mfululizo kwenye solistasi ya Desemba, mnamo tarehe 21 au 22. Latitudo yake unabadilika kidogo mara kwa mara pamoja na kucheza kwa mhimili wa mzunguko wa Dunia.

Maana ya mzingo aktiki[hariri | hariri chanzo]

Maana kwenye siku ya solistasi ya Desemba (mnamo 21 Desemba), Jua halitui tena chini ya upeo wa macho ndani ya mzingo aktiki hata saa za usiku wa manane. Kadiri latitudo inavyopungua, yaani tukielekea zaidi kwenda kusini na kukaribia ncha, kipindi cha mchana kinarefuka hadi kufikia nusu mwaka nchani kabisa.

Kinyume chake, ndani ya mzingo antaktiki kwenye siku ya solistasi ya Juni (mnamo 21 Juni), Jua halichomozi tena juu ya upeo. Hii haimaanishi giza kabisa wakati wa mchana lakini hakuna zaidi ila nuru ya mapambazuko saa 6 mchana. Kadiri tunavyokaribia ncha yaani kufika kusini, kipindi cha usiku na giza kabisa hurefuka hadi kufikia nusu mwaka nchani kabisa.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Mzingo antaktiki una urefu wa kilomita 16,000 hivi. [2] Maeneo ndani yake ni takribani kilomita za mraba 20,000,000 ambayo sawa na asilimia 4 za uso wa Dunia. [3]

Mzingo Aktiki hupita kwa jumla katika Bahari ya Kusini isipokuwa inagusa pia sehemu chache kwenye kaskazini ya Bara ya Antaktiki. Sehemu kubwa ya Antaktiki ziko ndani ya mzingo huu. Hakuna vijiji au miji na hivyo hakuna wakai wa kudumu ndani ya mzingo antaktiki, isipikuwa vituo kadhaa vya kisayansi na wafanyakazi wao.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Obliquity of the Ecliptic, Nutation in Obliquity and Latitudes of the Arctic/Antarctic Circles, tovuti ya NeoProgrammics PHP Science Labs, Basic Astronomy and Science-Related Tools, iliangaliwa Septemba 2019
  2. Nuttall, Mark (2004). Encyclopedia of the Arctic Volumes 1, 2 and 3. Routledge. uk. 115. ISBN 978-1579584368. Iliwekwa mnamo 26 Julai 2016.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Marsh, William M.; Kaufman, Martin M. (2012). Physical Geography: Great Systems and Global Environments. Cambridge University Press. uk. 24. ISBN 978-0-521-76428-5.