Mwili wa mwanadamu
Mandhari
Mwili wa mwanadamu ni muundo mzima wa mwanadamu upande wa mwili, bila kuzingatia roho inayoweza kuuhuisha.
Unajumuisha aina mbalimbali za seli ambazo zinajumuika pamoja na tishu na mifumo ya viungo vingine, kama vile kichwa, shingo, kiwiliwili (ambayo ni pamoja na kifua na tumbo), mikono na miguu.
Utafiti wa mwili wa binadamu unahusisha anatomia, fiziolojia, histolojia na embriolojia. Fiziolojia inazingatia mifumo na viungo vya mwili wa binadamu na kazi zake.
Mifumo mingi huingiliana ili kudumisha homeostasis, na viwango salama vya vitu kama sukari na oksijeni katika damu.
Makala hii kuhusu mambo ya anatomia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mwili wa mwanadamu kama matumizi yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |