Muhammed Said Abdulla

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Muhammed Said Abdulla (25 Aprili, 1918 - Machi 1991) ni mwandishi kutoka nchi ya Tanzania katika visiwa vya Zanzibar. Historia fupi katika maisha yake ambayo ilikuwa ni kumbukumbu isiyofutika katika uhai wake ni kuuliwa kwa familia yake, mkewe na watoto wake wawili wa kike waliouawa katika kipindi cha mapinduzi ya Zanzibar. Hasa anajulikana kwa hadithi zake za upelelezi ambazo mhusika wao mkuu ni Bwana Msa. Baadhi yao ni:

Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Abdulla alikuwa ni mhariri na mwaandishi wa vitabu tofauti ambavyo viliinyanyua lugha ya kiswahili katika daraja la juu na kuiongezea umaarufu mkubwa eneo la afrika mashariki. Alifanikiwa kuowa mke na kupata wawili katika maisha yake. Vile vile ni miongoni mwa watetezi wakubwa walifanya utetezi katika kuikomboa nchi ya Zanzibar kutoka mikononi mwa Watanganyika. Na hii ndio ilikuwa sababu ya yeye kuwa katika hatari ya maisha yake. Miongoni mwa beti zake za kuwatupia watanganyika ujumbe utakaoweza kuwapotezea nguvu ya kutaka kuinyakuwa Zanzibar. Njama ilianza kupangwa na watanganyika ili kumuondoa Bwana Msa Katika hii dunia. Aliuwawa yeye na familia yake, mkewe na watoto wake wawili wa kike katika kipindi cha mapinduzi ya Zanzibar. Hili lilikuwa pigo kubwa sana kwa Wazanzibari wote kwa kuuwawa Bwana Msa katika mazingira ya kutatanisha.


Inkwell icon - Noun Project 2512.svg Makala hii kuhusu mwandishi fulani wa Afrika bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Muhammed Said Abdulla kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.