Mtumiaji:Jackson Mujungu/Vanessa Arauz

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Vanessa Arauz[hariri | hariri chanzo]

Vanessa Arauz mnamo mwaka 2018

Vanessa Arauz León (alizaliwa mnamo tarehe 5 Februari mwaka 1989) ni meneja wa mpira wa miguu wa Ekuador ambaye alikuwa kocha mkuu wa timu ya wanawake ya Colo-Colo ya nchini Chile hadi 2020. Alikuwa kocha mkuu wa Ekuador katika Kombe la Dunia la Wanawake la FIFA mnamo mwaka 2015 akiwa na umri wa miaka 26, aliajiriwa akiwa na umri wa miaka 24, na kuweka rekodi ya dunia kwa kuwa kocha mwenye umri mdogo zaidi katika Kombe la Dunia la FIFA la Wanaume au Wanawake.[1] Katika Kombe la Dunia la FIFA la mwaka 2015, Ekuador walimaliza wa mwisho, wakifunga bao moja pekee. Ingawa mashirikisho mengi huenda yangelimfukuza kocha baada ya kufunga mabao machache kiasi hicho, haswa kocha wa kike. Jambo la kushangaza ni kwamba shirikisho liliamua kubakia na Arauz kwa mpango wa kitaifa wa wanawake katika ngazi zote. Kufikia mwaka 2017, alikuwa akifundisha timu zote za wanawake za shirikisho na aliteuliwa kuwa mwalimu rasmi na CONMEBOL. Katika nafasi hiyo, Arauz alisafiri kutoa usaidizi na mafunzo kwa programu za wanawake Amerika Kusini kote. Kupitia juhudi za shirikisho, Arauz alithibitika kuwa uso wa mabadiliko ndani ya Amerika ya Kusini na haki za wanawake, haswa ndani ya mpira wa miguu.[2]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Ecuador's 26-year-old coach claims new record at FIFA Women's World Cup". Guinness World Records (kwa en-gb). 2015-06-09. Iliwekwa mnamo 2022-12-11. 
  2. author, Elsey, Brenda,. Futbolera : a history of women and sports in Latin America. ISBN 1-4773-1858-5. OCLC 1352452652.