Mtumiaji:ChriKo
Lugha | ||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|
|
Jina langu ni Christiaan Kooyman. Nimezaliwa nchini Uholanzi ambapo nilisomea ekolojia kwenye Chuo Kikuu cha Kilimo cha Wageningen (sikuhizi Wageningen University and Research Centre). Baada ya mahafali yangu ya Shahada ya uzamili nilihamia Afrika ambapo nimefanya kazi tokea hapo katika nchi nyingi (nchi za makazi: Nijeria, Kenya, Sudani, Nijeri, Benin, Senegali na Maroko). Takriban kazi zangu zote zilihusisha vipengele vya entomolojia. Tangu mwaka 1996 ninajiona kama mwanaentomopatholojia (mwanapatholojia ya wadudu). Kazi yangu kwa sasa ni mshauri wa kifundi katika idara ya Uchunguzi na Usitawishaji ya Eléphant Vert, kampuni ya kutengeneza dawa za kibiolojia na mbolea wa kibiolojia huko Meknès, Maroko. Ni mkuu wa idara ndogo ya dawa za kibiolojia ambamo tunasitawisha dawa zilizo na spora za kuvu entomopathojeni ndani yake.
Habari zako? Ukiwa mtaalamu wetu wa viumbe hai - labda jaribu hii: http://news.bbc.co.uk/2/hi/science/nature/4759535.stm --Kipala 19:07, 12 May 2006 (UTC)
Asante, nimefuraha kuona hii, ni ya ajabu. ChriKo 12:49, 26 May 2006 (UTC)
ChriKo, unakaribishwa kujiunga kwenye kikundi cha mazungumzo kuhusu mawikipedia ya lugha mbalimbali za Kiafrika. Naomba utembelee http://groups.yahoo.com/group/afrophonewikis/ kujiandiksha. Asante, Malangali 19:35, 16 Agosti 2006 (UTC)