Nenda kwa yaliyomo

Gambia (mto)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mto Gambia)
Mto Gambia
Mto Gambia kutoka angani - mstari mweusi ni mipaka ya nchi ya Gambia.
Chanzo Nyanda za juu za Futa Djalon, Guinea
Mdomo Atlantiki kwa mji wa Banjul
Nchi Guinea, Senegal & Gambia
Urefu 1,120 km
Kimo cha chanzo 900 m takriban
Mkondo hadi 2000 m³/s kutegemeana na majira na kiasi cha mvua njiani
Eneo la beseni 69,931 hadi 87,850 km² (maelezo hutofautiana)

Gambia ni mto unaoanza katika milima ya Futa Djalon huko Guinea. Unafuata njia ya kunyoka hadi Atlantiki. Mdomo wake ni pana sana.

Baada ya kutoka katika Futa Djallon mto unaelekea kaskazini-magharibi kupitia mkoa wa Tambakunda katika Senegal halafu mbuga wa wanyama wa Niokolo Koba. Hapa inapokea tawimiti ya Nieri Ko and Kuluntu na kuingia katika nchi ya Gambia karibu na mji wa Fatoto.

Mto Gambia ukipitia mbuga wa Niokolo-Koba nchini Senegal

Kuanzia hapa mto unaelekea magharibi tu isipokuwa kwa njia ya kunyokanyoka. Takriban km 100 kabla ya kufika mdomo unaanza kupanuka ukiwa na upana wa km 10 mdomoni penyewe.

Mto una visiwa mbalimbali ndani yake, vikubwa zaidi ni kisiwa cha Tembo na kisiwa cha MacCarthy. Kisiwa cha James Island mdomoni kabisa kilikuwa kituo muhimu cha biashara ya watumwa na kimeandikishwa katika orodha ya UNESCO ya Urithi wa Dunia.

Kutokana na upana na wingi wa maji Gambia inafaa kama njia ya maji; meli za baharini zinaingia ndani takriban km 280.

Miji mikubwa zaidi mtoni ni Basse Santa Su, Janjanbureh na Banjul.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]

en: The Gambia Basin Ilihifadhiwa 10 Mei 2006 kwenye Wayback Machine.