Nenda kwa yaliyomo

Mtapenda

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Kata ya Mtapenda
Nchi Tanzania
Mkoa Mkoa wa Katavi
Wilaya Wilaya ya Nsimbo
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 9,277

Mtapenda ni kata mojawapo kati ya 12 zinazounda Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo iliyoko katika Mkoa wa Katavi, Tanzania. Kata hiyo ndiko zilipo ofisi za makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo, pia inajulikana kutokana na kuwa na eneo maalumu lililotengwa kwa ajili ya shughuli za uwekezaji wa viwanda. Ina postikodi namba 50118.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 9,277 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 4,811 waishio humo.[2]

Ni kata yenye wakazi wa makabila mchanganyiko wanaozungumza lugha mbalimbali kama vile Kifipa, Kibende, Kirwila, Kikonongo na nyinginezo, ila Wafipa ndio waliotawala sana maeneo haya.

Kijiji cha Mtapenda kina idadi kubwa ya wanywaji wa pombe ya kienyeji.

Kata za Wilaya ya Nsimbo - Mkoa wa Katavi - Tanzania

Ibindi | Itenka | Kanoge | Kapalala | Katumba | Litapunga | Machimboni | Mtapenda | Nsimbo | Sitalike | Ugalla | Uruwira


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Katavi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.