Nenda kwa yaliyomo

Mtango-tamu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mtango-tamu
(Solanum muricatum)
Mtango-tamu
Mtango-tamu
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Plantae (Mimea)
(bila tabaka): Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
(bila tabaka): Eudicots (Mimea ambayo mche wao una majani mawili)
(bila tabaka): Asterids (Mimea kama alizeti)
Oda: Solanales (Mimea kama mnavu)
Familia: Solanaceae (Mimea iliyo na mnasaba na mnavu)
Jenasi: Solanum
Spishi: S. muricatum
Ait.

Mtango-tamu (Solanum muricatum) ni mmea wa familia Solanaceae. Ijapokuwa mmea huu una mnasaba na mnyanya, matunda yake, yaitwayo matango matamu, yana ladha tofauti kabisa. Matunda haya yanafanana na magogwe makubwa na ladha yao ni mchanganyiko wa tikiti-asali na tango.

Mitango-tamu hukuzwa kwa biashara nchini Chili, Australia ya Magharibi na Nyuzilandi hasa, lakini pia katika Kolombia, Peru, Ekwador, Hispania, Kenya, Maroko na Marekani.

Picha[hariri | hariri chanzo]