Mradi wa Jenomu ya Binadamu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nembo ya Mradi wa Jenomu ya Binadamu

Mradi wa Jenomu ya Binadamu (kwa Kiingereza: Human Genome Project) ulikuwa mradi wa utafiti wa kisayansi wa kimataifa uliolenga kutambua jozi za besi ambazo zinaunda ADN ya binadamu, na kutengeneza ramani yote ya jeni za jenomu ya binadamu katika mtazamo wa mwili na utendaji. [1] Bado ni mradi mkubwa zaidi wa kibaiolojia ulioshirikisha ulimwengu.[2]

Mipango ilianza baada ya wazo hilo kuchukuliwa na serikali ya Marekani mwaka 1984, mradi huo ulizinduliwa rasmi mnamo 1990, na ulitangazwa kuwa kamili mnamo Aprili 14, 2003.[3] Kiwango cha jenomu kamili kilifanikiwa mnamo Mei 2021. [4][5]

Ufadhili ulitoka kwa serikali ya Marekani kupitia Taasisi za Kitaifa za Afya (kwa Kiingereza: National Institutes of Health (NIH)) na vilevile vikundi vingine vingi kutoka ulimwenguni kote. Mradi unaofanana na huu ulifanywa nje ya serikali na Shirika la Celera, au Celera Genomics, ambayo ilizinduliwa rasmi mnamo 1998. Katika kutambua mlolongo wa jozi za besi, tafiti nyingi zilizofadhiliwa na serikali zilifanywa katika vyuo vikuu ishirini na vituo vya utafiti huko Marekani, Uingereza, Japan, Ufaransa, Ujerumani, na China.[6]

Mradi wa Jenomu ya Binadamu hapo awali ulilenga kutengeneza ramani ya nyukleotidi zilizomo kwenye jenomu ya rejeleo lenye seti moja ya chembeuzi za binadamu (zilizo zaidi ya bilioni tatu). Jenomu ya kila mtu ni ya pekee; kupanga ramani ya jenomu ya binadamu kulihusisha kutafiti mlolongo wa ADN katika idadi ndogo ya watu na kisha kukusanya taarifa hizo ili kupata mlolongo kamili kwa kila chembeuzi. Kwa hiyo, jenomu ya binadamu iliyomalizika ni mozaiki kwa sababu ina mchanganyiko wa taarifa za seli kutoka kwa zaidi ya mtu mmoja, haimwakilishi mtu yeyote maalumu. Manufaa ya mradi huo yanatokana na ukweli kwamba sehemu kubwa ya jenomu ya binadamu ni sawa kwa wote.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]