Modafinil
Modafinil (huuzwa kwa jina la Provigil miongoni mwa dawa nyingine) ni dawa ya kutibu usingizi kutokana na sababu mbalimbali kama vile narcolepsy. Utafiti juu ya ufanisi wake kwa matumizi hayo bado haujakamilika.[1][2] Dawa hii huwa inachukuliwa kwa kinywa.
Madhara ya kawaida ni pamoja na maumivu ya kichwa, wasiwasi, shida ya kulala, na kichefuchefu. Madhara makubwa yanaweza kujumuisha athari kama vile anaphylaxis, ugonjwa wa Stevens-Johnson, au njozi. Haijulikani ikiwa matumizi wakati wa ujauzito ni salama. Kiasi cha dawa kinachotumiwa kinahitaji kubadilishwa kwa walio na matatizo ya figo au ini. Haipendekezwi kwa wale wenye Shinikizo la juu la damu.
Jinsi inavyofanya kazi si wazi kabisa. Uwezekano mmoja ni kwamba inaweza kuathiri maeneo ya ubongo yanayohusika na mzunguko wa usingizi.
Modafinil iliidhinishwa kwa matumizi ya matibabu nchini Marekani mwaka 1998.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Battleday RM, Brem AK (Novemba 2015). "Modafinil for cognitive neuroenhancement in healthy non-sleep-deprived subjects: A systematic review". European Neuropsychopharmacology. 25 (11): 1865–81. doi:10.1016/j.euroneuro.2015.07.028. PMID 26381811.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Meulen, Ruud ter; Hall, Wayne; Mohammed, Ahmed (2017). Rethinking Cognitive Enhancement (kwa Kiingereza). Oxford University Press. uk. 116. ISBN 9780198727392.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- RxList Patient Information Ilihifadhiwa 30 Desemba 2006 kwenye Wayback Machine. for modafinil users
- U.S. National Library of Medicine: Drug Information Portal – Modafinil
- Matumizi na madhara ya modafinil toka WEBMD
- Utafiti wa kitaaluma kuhusu madhara ya modafinil
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Modafinil kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |