Nenda kwa yaliyomo

Mkonje

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mkonje
Mkonje dorabi (Chirocentrus dorab)
Mkonje dorabi (Chirocentrus dorab)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Actinopterygii
Oda: Clupeiformes
Familia: Chirocentridae
Cuvier & Valenciennes, 1846
Jenasi: Chirocentrus
Cuvier, 1816
Ngazi za chini

Spishi 2:

Mikonje, mikonge au panga ni spishi mbili za samaki wa baharini katika jenasi Chirocentrus ya familia Chirocentridae na oda Clupeiformes. Wana nasaba na dagaa.

Spishi zote mbili zina mwili uliorefuka na mataya yenye meno marefu makali ambayo huwezesha hamu yao kubwa, hasa kwa samaki wengine. Hufikia urefu wa m 1. Wana mbavu za rangi ya fedha na mgongo wa kibuluu.

Mikonje huvuliwa kwa kibiashara na kuuzwa wabichi au waliogandishwa.

  • Rashid Anam & Edoardo Mostarda (2012) Field identification guide for the living marine resources of Kenya. FAO, Rome.
  • Gabriella Bianchi (1985) Field guide to the commercial marine brackish-water species of Tanzania. FAO, Rome.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkonje kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.