Nenda kwa yaliyomo

Jimbi (ngeli ya mimea)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mkangaga)
Jimbi
Jimbi manyoya (Cheilanthes hirta)
Jimbi manyoya (Cheilanthes hirta)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Plantae (Mimea)
(bila tabaka): Tracheophytes (Mimea iliyo na vifereji)
Ngeli: Polypodiopsida (Mimea isiyotoa mbegu lakini spora)
Cronquist, Takht. & W.Zimm.
Ngazi za chini

Nusungeli 4 na oda 11 zilizopo bado:

Mimea mingi yenye vifereji huunda maua na mbegu kwa uzazi. Walakini, kikundi kikubwa cha mimea katika ngeli Polypodiopsida haitoi hata moja wala nyingine. Wanazaa kupitia uundaji wa spora. Hizi mara nyingi hufanyika katika vikundi, vinavyoitwa sori (sorus), kwenye upande wa chini wa majani. Kwa Kiingereza mimea hiyo huitwa ferns kwa ujumla. Katika Kiswahili kuna majina mbalimbali yanayotumika, kama jimbi, dege la watoto, madole matano na (m)kangaga. Kwa kuwa jimbi hutumika kwa “ferns” zilizo kawaida sana katika Afrika ya Mashariki, inapendekezwa kutumia jina hili kama jina la jumla. Madege ya watoto inafanana na majimbi, lakini madole matano inamea juu ya miti au miamba na kwa hatua fulani huwa na majani karibu matano katika kila tawi. Kangaga ina matawi marefu sana na mara nyingi mashina kama miti.

Kwa kawaida wanasayansi huita sehemu zilizo juu ya ardhi fronds, kama matawi au makuti ya mitende. Katika makala hii istilahi matawi itatumiwa. Kwa kawaida kila tawi hubeba majani mengi ambayo yanaweza kugawanywa katika vijani. Walakini, matawi pia inaweza kuwa na jani moja.