Mjenzi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Construction Workers.jpg
Construction worker.jpeg
69 Fisk IRT work vests jeh.jpg
Matunda ya kazi ya wajenzi.

Mjenzi (kutoka kitenzi "kujenga", ambacho kwa asili kinahusu nyumba za miti, lakini sasa aina zote za majengo) ni mtu ambaye amebobea katika mambo ya ujengaji wa majengo ya aina mbalimbali kama nyumba, hata za maghorofa, shule, hospitali, maabadi, madaraja na mengineyo.

Mjenzi hutumia zana mbalimbali kujengea. Zana hizo ni kama vile tindo, nyundo, sepeto na vifaa vya kujengea kama miti, udongo, sementi, chokaa, mchanga na vinginevyo.

Siku hizi mjenzi kwa kawaida anafuata ramani ambayo imechorwa na mhandisi halafu imepitishwa na mamlaka ya serikali, ili kujenga vitu kwa vipimo na mahesabu.

Blank template.svg Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mjenzi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.