Milima ya Anatolia Kaskazini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ramani ya Anatolia: Milima ya Anatolia Kaskazini ni ile upande wa kusini wa Bahari Nyeusi.
Demirkazik Dagi iko mita 3756 juu ya UB.

Milima ya Anatolia Kaskazini ni safu ya milima katika Uturuki. Inafuatana na pwani ya Bahari Nyeusi upande wa kaskazini wa rasi ya Anatolia kwa urefu wa kilomita 1,000 hivi.

Jina la kihistoria la eneo hili ni "Ponto" kwa hiyo milima huitwa vile kwa lugha za Ulaya, k.m. "Pontic Mountains" kwa Kiingereza.

Safu hii ni milima kunjamano yenye mwelekeo wa magharibi - mashariki kwa upana wa km 100-200 kutoka pwani. Upande wa magharibi milima haina kimo kirefu lakini upande wa mashariki urefu wa milima unapita mita 3,000 na kukaribia 4,000 kabla ya kuishia kwenye mpaka wa Georgia.

Upande wa kaskazini wa milima unaotazama bahari hupokea mvua nyingi. Huko kuna misitu minene na kwenye mabonde kinastawi kilimo cha matunda na kokwa za hazel; sehemu hii ya Uturuki huzalisha theluthi mbili za hazel duniani[1].

Upande wa kusini ni yabisi.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. FAOSTAT crops ,search:Hazelnut with shells, 2017, tovuti ya FAO, iliangaliwa Novemba 2019
Makala hii kuhusu maeneo ya Uturuki bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Milima ya Anatolia Kaskazini kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.