Mikronesia
Mandhari
(Elekezwa kutoka Micronesia)
Mikronesia ni eneo la Bahari ya Pasifiki. Ni moja kati ya makundi makubwa matatu ya visiwa vya Pasifiki pamoja na Melanesia na Polynesia.
Jina limeundwa na maneno ya Kigiriki ya νῆσος (kisiwa) na μικρος (kidogo) yaani "visiwa vidogo". Mpelelezi na nahodha Mfaransa Jules Dumont d'Urville alitunga jina hili 1832 kwa kuweka uzito kwa udogo wa visiwa hivi vinavyozidi 2,000.
Mikronesia iko upande wa mashariki wa Ufilipino na upande wa kaskazini ya Guinea Mpya na Melanesia to the south, halafu magharibi ya Polynesia. Eeno lake ni klaskazini ya ikweta.
Nchi za Mikronesia
[hariri | hariri chanzo]Kisiasa kuna maeneo nane katika Mikronesia:
- Shirikisho la Mikronesia lenye majimbo manne: Kosrae, Yap, Pohnpei na Chuuk;
- Visiwa vya Bougainville (vinavyojitegemea ndani ya nchi ya Papua Guinea Mpya);
- Visiwa vya Marshall;
- Palau;
- Nauru;
- Kiribati;
- Visiwa vya Mariana ya Kaskazini (chini ya Marekani);
- Guam (eneo la Marekani).
- kisiwa cha Wake (kituo cha kijeshi cha Marekani).
Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.
|