Nenda kwa yaliyomo

Mgobi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mgwana)
Mgobi
(Canavalia rosea)
Mgobi kwenye pwani
Mgobi kwenye pwani
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Plantae (Mimea)
(bila tabaka): Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
(bila tabaka): Eudicots (Mimea ambayo mche wao una majani mawili)
(bila tabaka): Rosids (Mimea kama mwaridi)
Oda: Fabales (Mimea kama mharagwe)
Familia: Fabaceae (Mimea iliyo na mnasaba na mharagwe)
Nusufamilia: Faboideae (Mimea inayofanana na mharagwe)
Jenasi: Canavalia
Spishi: C. rosea
(Sw.) DC.

Mgobi, mgarara au mgwana (Canavalia rosea) ni mmea wa mazao wa nusufamilia Faboideae katika familia Fabaceae. Spishi hii inafanana na mbwanda (C. gladiata) lakini inamea karibu na ufuko katika mchanga takriban safi. Maua ni pinki na makaka ni mafupi na mapana zaidi. Mbegu zake huitwa magobi.

Mgobi hukua pwani za ukanda wa tropiki na unaweza kuhimili kitembo kiasi cha chumvi. Makaka yanaweza kuelea juu ya maji na kwa hiyo yamesambaa kwenye pwani zote za tropiki. Pengine mmea huu hukuzwa juu ya matuta ili kuamirikisha mchanga.

Makala hii kuhusu mmea fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mgobi kama uainishaji wake wa kibiolojia, uenezi au matumizi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.