Nenda kwa yaliyomo

Mfuko wa backpack

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mwanajeshi akiwa amevaa mfuko wa backpack wa kijeshi mgongoni

Backpack ni aina ya mfuko uliotengenezwa kwa kitambaa na ambao huwa na mikanda miwili ambayo husaidia mwenye begi hii kuubeba kwa nyuma. Mfuko wa backpack huonekana kwa wanafunzi wanapobeba vitabu, kwa wanaokwenda kwa ziara tofautitofauti (travelers) wakiwa wamebeba mizigo yao. Wanaokwea milima hupenda mfuko huu ambao huwawezesha kubeba nguo, vyakula na hata magodoro ya kulalia.

Kuna majina tofauti ya mfuko huu kama carry on backpack, rucksack na pia knapsack. Jina backpack lilianzia nchini Amerika mwakani 1910.

Badala ya kubebea mizigo mizito kwa begi ya mkono (handbag), watu hupenda kubeba mizigo yao kwa nyuma maana hali hii huwawezesha kubeba mizigo mingi zaidi.

mfuko wa backpack

Mfuko wa backpack haswa kwa wanaokwenda ziara huwawezesha kubeba hadi kilo kumi katika mifuko hii.

Sanaa za mfuko wa backpack

Watengenezaji wa backpack huweza wakabuni sanaa tofauti kwa kutengeneza begi hizi.

Hii ni kama:

  • Begi zisizo na fremu (frameless)
  • Begi zilizo na fremu ya nje (external frame
  • Begi zilizo na fremu ya ndani (internal frame)

Fremu husaidia kugawanya uzito wa mzigo kwa mfuko wote ili kusiwe na uzito mahala pamoja tu. Haswa fremu huweka uzito kwa miguu ya mbebaji na kuutoa kwa mabega ili asiende akaumia kwa uzito mwingi.

Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mfuko wa backpack kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.