Wafilisti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mfilisti)
Miji mitano ya Wafilisti: Gaza, Ashdod, Askalona, Ekron, na Gath.

Wafilisti (kwa Kiebrania: Plištim, "watu wa Plešt": jina hilo linapatikana mara 286 katika Biblia ya Kiebrania, kati yake mara 152 katika 1 Sam) walikuwa kabila la watu wa Ulaya Kusini Mashariki ambao walivuka Bahari ya Kati.

Kisha kushindwa kuvamia Misri waliteka pwani ya Kanaani (1175 KK hivi) wakifaidika na silaha za chuma walizozitumia dhidi ya watu waliokuwa na zile za shaba tu, wakiwa wenyeji au Waisraeli.

Ingawa hawakuwa wengi, waliathiri sana nchi yao mpya, kiasi cha kuiachia jina la Palestina.

Habari nyingi juu yao zinapatikana katika Biblia.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Marejeo mengine[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wafilisti kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.