Nenda kwa yaliyomo

Meroë

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Meroe ni kivutio cha kiutamaduni nchini Sudan. Kati ya piramidi zilizopo, nyingi ni maghofu.

Meroë (kwa Kimeroe: Medewi au Bedewi) ni jina la mji wa kale. Mabaki ya majengo yake yanapatikana kwenye ukingo wa mashariki wa mto Nile karibu kilomita 6 kaskazini mashariki mwa Kabushiya karibu na Shendi, nchini Sudan. Meroe iko mnamo kilomita 200 kaskazini mashariki mwa Khartoum kando ya barabara kuu kutoka Khartoum kuelekea Atbara. Karibu kuna vijiji vichache ambavyo vinaitwa Bagrawiyah.

Meroë ilikuwa mji mkuu wa Ufalme wa Kushi kwa karne kadhaa. [1]

Urithi wa Dunia[hariri | hariri chanzo]

A modern satellite view of the region of Meroe (October 2020).

Tangu Juni 2011 eneo la Meroe limeandikishwa katika orodha ya UNESCO inayotaja "Urithi wa Dunia.[2]

Meroe inajulikana kwa piramidi zake nyingi. Piramidi hizo si kubwa kama zile za Gizah katika Misri lakini idadi ni kubwa, kwa jumla zilikuwa zaidi ya 200.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. [1]
  2. Archaeological Sites of the Island of Meroe, tovuti ya Unesco, iliangaliwa Januari 2021
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Meroë kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.