Nenda kwa yaliyomo

Medard Matogolo Kalemani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Medard Kalemani)
Mh Medard Kalemani


Waziri wa Nishati
Muda wa Utawala
7 October 2017 – 2020

Aliingia ofisini 
November 2015

tarehe ya kuzaliwa 15 March 1968
utaifa Mtanzanaia
chama CCM
mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Medard Matogolo Kalemani (amezaliwa 15 Machi 1968) ni mwanasiasa Mtanzania na mwanachama wa Chama cha kisiasa cha Chama Cha Mapinduzi (CCM). Amechaguliwa kuwa Mbunge wa Chato kuanzia mwaka 2015 hadi 2020. [1]

Kuhusu Elimu

[hariri | hariri chanzo]

Medard M. Kalemani alianza masomo ya msingi katika Shule ya Msingi Nyambogo mnamo mwaka 1978 na kumaliza darasa la saba mwaka 1984, mwaka 1985 alifanikiwa kujiunga na shule ya sekondari ya Kashororo mpaka mwaka 1988 ambapo alifanikiwa kuendelea na masomo ya juu ya Sekondari kuanzia mwaka 1989 hadi 1991 katika Shule ya Sekondari ya Milambo. Kuanzia mwaka 1993 hadi mwaka 1996 alifanikiwa kupata Shahada ya Awali ya Sheria (LLB) katika Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Mwaka 2000 hadi 2002 alijinyakulia cheti cha Shahada ya Uzamili (LLM) kwenye sekta ya Madini na Nishati kutoka Chuo Kikuu cha Dundee, Medard M. Kalemani hakuishia hapo kwani mnamo mwaka 2002 hadi 2006 alisoma tena katika Chuo Kikuu cha Bedford, UK na kutunukiwa Shahada ya Uzamivu (Phd) na kwakuzingatia elimu yake hiyo kwa sasa anaitumikia kama Waziri wa Nishati kwa dhamana aliyopewa na Rais Wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.

  1. Tovuti ya Bunge la Tanzania, iliangaliwa Mei 2017