Matandu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Matandu
Matandu kusi (Aparallactus capensis)
Matandu kusi (Aparallactus capensis)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Reptilia (Wanyama wenye damu baridi na magamba ngozini)
Oda: Squamata (Mijusi, mijusi-nyungunyungu na nyoka)
Nusuoda: Serpentes (Nyoka)
Familia: Lamprophiidae (Nyoka walio na mnasaba na chata)
Fitzinger, 1843
Nusufamilia: Aparallactinae (Nyoka wanaofanana na matandu)
Bourgeois, 1968
Jenasi: Aparallactus
A.Smith, 1849
Ngazi za chini

Spishi 11:

Matandu ni nyoka wenye sumu wa jenasi Aparallactus katika familia Lamprophiidae. Wamepewa jina hili kwa sababu hula tandu.

Nyoka hawa ni wafupi na wembamba, sm 55 kwa kipeo lakini chini ya sm 40 kwa kawaida. Rangi yao ni nyeusi, kijivu au kahawia. Wale wenye rangi kahawia wana kichwa cheusi na/au baka jeusi shingoni kwa kawaida.

Matandu huishi katika vishimo, katika udongo tebwere au chini ya takataka za majani ambapo huwinda tandu.

Chonge ni meno ya nyuma na hizi ni ndefu kulingana na ukubwa wao kuliko chonge za spishi nyingine za familia Lamprophiidae. Lakini matandu magharibi hana chonge. Kwa sababu ya udogo wao wengi hawawezi kung'ata watu lakini hata waking'ata hawawezi kuleta hasara nyingi.

Spishi[hariri | hariri chanzo]

Picha[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Spawls, S., Howell, K., Drewes, R. & Ashe, J. (2002) A field guide to the Reptiles of East Africa. Academic Press, San Diego, CA, USA.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Matandu kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.