Matandu
Mandhari
(Elekezwa kutoka Aparallactus)
Matandu | ||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Matandu kusi (Aparallactus capensis)
| ||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
| ||||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||||
Spishi 11:
|
Matandu ni nyoka wenye sumu wa jenasi Aparallactus katika familia Lamprophiidae. Wamepewa jina hili kwa sababu hula tandu.
Nyoka hawa ni wafupi na wembamba, sm 55 kwa kipeo lakini chini ya sm 40 kwa kawaida. Rangi yao ni nyeusi, kijivu au kahawia. Wale wenye rangi kahawia wana kichwa cheusi na/au baka jeusi shingoni kwa kawaida.
Matandu huishi katika vishimo, katika udongo tebwere au chini ya takataka za majani ambapo huwinda tandu.
Chonge ni meno ya nyuma na hizi ni ndefu kulingana na ukubwa wao kuliko chonge za spishi nyingine za familia Lamprophiidae. Lakini matandu magharibi hana chonge. Kwa sababu ya udogo wao wengi hawawezi kung'ata watu lakini hata waking'ata hawawezi kuleta hasara nyingi.
Spishi
[hariri | hariri chanzo]- Aparallactus capensis, Matandu Kusi (Cape centipede-eater)
- Aparallactus guentheri, Matandu Mweusi (Black centipede-eater)
- Aparallactus jacksoni, Matandu wa Jackson (Jackson's centipede-eater)
- Aparallactus lineatus, Matandu Milia (Lined centipede-eater)
- Aparallactus lunulatus, Matandu Kijivu (Plumbeous centipede-eater)
- Aparallactus modestus, Matandu Magharibi (Western forest centipede-eater)
- Aparallactus moeruensis, Matandu wa Kongo (Zaire centipede-eater)
- Aparallactus niger, Matandu Mweusi Magharibi (Western black centipede-eater)
- Aparallactus nigriceps, Matandu wa Msumbiji (Mozambique centipede-eater)
- Aparallactus turneri, Matandu wa Malindi (Malindi centipede-eater)
- Aparallactus werneri, Matandu wa Usambara (Usambara centipede-eater)
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Matandu kijivu mchanga
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Spawls, S., Howell, K., Drewes, R. & Ashe, J. (2002) A field guide to the Reptiles of East Africa. Academic Press, San Diego, CA, USA.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Matandu kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |