Makrina Mkubwa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Makrina Mzee)

Makrina Mkubwa (kabla ya 270 - 340 hivi) alikuwa mwanamke mlei mwenye imani ya Kikristo katika eneo la katikati ya Uturuki wa leo.

Ni maarufu hasa kama mama wa Basili Mzee, na bibi wa Basili Mkuu, Gregori wa Nisa, Petro wa Sebaste na Makrina Mdogo.[1]

Anaheshimiwa kama mtakatifu na msimamizi wa wajane na wa mapambano dhidi ya ufukara. Sikukuu yake inaadhimishwa tarehe 14 Januari.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Basili Mkuu aliandika kwamba alifundishwa na Gregori Mtendamiujiza, na kwa njia yake athari ya mtakatifu huyo iliwafikia yeye na ndugu zake.[2]

Nyumba yake ilikuwa huko Kaisarea Mpya katika mkoa wa Ponto ila wakati wa dhuluma za makaisari Galerius na Diocletianus dhidi ya Wakristo, Makrina na mumewe walikimbilia pwani ya Bahari Nyeusi.[2]

Inasemekana alifariki baada ya mume wake mwanzoni mwa miaka ya 340.[3]

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Attwater, Donald; John, Catherine (1995), "Macrina the Elder", The Penguin Dictionary of saints, London: Penguin Books, ISBN 978-0-14-051312-7, iliwekwa mnamo 2013-01-26 
  2. 2.0 2.1 Macrina the Elder, Saint, Philosopher, Grandmother of Macrina, iliwekwa mnamo 2013-01-26 
  3. Kirsch, Johann (1910), "St. Macrina the Elder", The Catholic Encyclopedia 9, New York: Robert Appleton Company, iliwekwa mnamo 2013-01-26 
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.