Makari wa Yerusalemu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mchoro mdogo kuhusu Mt. Makari na Ushindi wa Msalaba.

Makari wa Yerusalemu (alifariki 335 hivi) alikuwa askofu wa Yerusalemu kuanzia mwaka 312 hadi kifo chake[1].

Alishiriki Mtaguso wa kwanza wa Nisea (325) na kupinga Uario[2]. Kwa hiyo alisifiwa sana na Atanasi wa Aleksandria.

Pia alihimiza kaisari Konstantino Mkuu na mama yake Helena kuchimbua mahali patakatifu mjini Yerusalemu hata ukapatikana msalaba wa Yesu na baada ya hapo waliagiza mabasilika mahali pake (hasa Kanisa la Kaburi na Ufufuo wa Yesu)[3].

Tangu kale anaheshimiwa na Waorthodoksi na Wakatoliki kama mtakatifu[4][5].

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 10 Machi[6].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/44300
  2. Theodoret, "H. E.", I, 4.
  3. Eusebius, Vita Constantini, III, 28, 30-32; Theodoret, H. E., I, 16.
  4. https://catholicexchange.com/saint-macarius
  5. Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2020-09-28. Iliwekwa mnamo 2021-03-07.
  6. Martyrologium Romanum, 2004

Maandishi yake[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.