Makari wa Aleksandria (mfiadini)
Mandhari
Makari wa Aleksandria (alifia dini Aleksandria, Misri, 250 hivi) alikuwa Mkristo mwenye asili ya Libya ambaye aliuawa kikatili wakati wa dhuluma ya kaisari Decius.
Kisha kushawishwa na hakimu muda mrefu amkane Kristo, kwa kuwa Makari alizidi kukiri kwa imara imani yake, hakimu aliagiza achomwe moto akiwa hai [1].
Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki kama mtakatifu mfiadini.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 8 Desemba[2], lakini pia 30 Oktoba[3], kama si watu wawili tofauti[4].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |