Majadiliano ya mtumiaji:DANIEL DE SANTOS
Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!
Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.
Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na b) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.
Kwa mawili matatu labda tazama:
- Kuhusu ukurasa wako wa mtumiaji na kurasa nyingine
- Ukurasa wa mwongozo
- Jamii:Msaada (makala zilizomo humo zinaweza kusaidia mara nyingi)
- Ukurasa wa jumuia (pamoja na Wikipedia:Wakabidhi, penye majina walio tayari kukusaidia)
- Makala za msingi za Wikipedia
Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.
Ujue miiko:
- usilete kamwe matini wala picha kutoka tovuti za nje
- usiingize matangazo ya kibiashara (pamoja na kuelekeza kwa kurasa zenye matangazo).
- usimwage kamwe matini kutoka google-translate au programu za kutafsiri.
Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!
Welcome to Kiswahili Wikipedia!
We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:
- do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
- nor copied texts/images from other webs to this site!
- do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.
As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.
Kipala (majadiliano) 15:34, 16 Juni 2017 (UTC)
Habari ndugu, asante kwa kuendelea!! Naona numeanzisha makala kuhusu ukame. Basi kuna chanzo ingawa si makala nzuri bado makosa na kasoro, haiwezi kubaki jinsi ilivyo. Sasa naomba tushirikiane ili tufanye ukame kuwa makala inayofaa. Naomba twende pamoja. Fanya hatua zifuatazo:
- fanya neno la kwanza ("Ukame") kuonekana koze
- panga makala katika jamii. kuna jamii mbili ambazo ni Jamii:Metorolojia na pia Jamii:Maafa asilia. Kopi maneno koze hapo, ziweke chini ya makala kama kiungo
- unganisha makala na lugha nyingine. Hapo nenda chini kushoto kwa "Lugha" na chini yake kwa "Add links". Bofya hapo, utaona "Please select a site and a page that you want to link to this page. Language: ..."
- Katika nafasi ya "language" ingiza enwiki na chini yake kwa "page" ongeza drought. Utaona orodha ya maneno uthebitishe kwa click kwenye neno hilihili "drought". Sasa click "link with page" na uthebitishe tena.
- Baada ya kumaliza utaona orodha ya lugha upande wa kushoto wa dirisha (kama huoni bofya kwenye mshale mviringo juu katika dirisha la anwani, itafanya upya)
- Sasa nenda na tafuta kwenye lugha hadi unafika "simple English". (kama una matata kopi mstari unaofuata katika dirisha mpya / la pili)
- simple.wikipedia.org/wiki/Drought
- fungua makala ya Drought katika Simple English , soma na utaona kasoro za jaribio lako. Tafsiri unavyoweza au uongeze kwa maneno yako mwenyewe.
- Halafu unijibu kwenye ukurawa wangu wa majadiliano kama unakwama au kufaulu, umwonyeshe pia Nd. Riccardo ukimwona. Kipala (majadiliano) 15:34, 16 Juni 2017 (UTC)
- Salaamu sana, naomba usiendelee kuanzisha makala mapya, kwanza jaribu kuboresha moja. Bado hujaelewa namna gani kuandika na kuingiza hapa. Nilikupa msaada kwa ukame fuatilia hatua hizi. Tafadhali! Kipala (majadiliano) 14:10, 17 Juni 2017 (UTC)
Daniel, nimeshakuandikia hapo juu usiendelee kuanzisha makala mapya, rudia kuboresha kile ulichoandika tayari! Sasa naomba uniandikie kwenye ukurasa wangu Majadiliano ya mtumiaji:Kipala ya kwamba uliona na kuelewa ninachosema hapa. Halafu uangalie makala zako Nywele (fupi mno, hakuna jamii, hakuna kiungo kwa lugha nyingine). Unaweza kuiboresha kwa kusoma simple:Hair au sehemu ya kwanza ya en:Hair na kuchagua habari kadhaa ambazo umeelewa na kuyasema kwa Kiswahili. Halafu ukubuke kuweka viungo vya ndani. Baada ya kumaliza haya urudie pia Elfu moja na sita na Elfu moja na sita ambazo zote mbili hazina umbo zuri. Ukiwa na swali, uliza! Nitamwomba Nd Riccardo asisahihishe jinsi alivyofanya awali tuone ya kwamba utafaulu mwenyewe. Kipala (majadiliano) 08:24, 17 Julai 2017 (UTC)