Majadiliano ya mtumiaji:20 Savage
Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!
Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.
Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na b) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.
Kwa mawili matatu labda tazama:
- Kuhusu ukurasa wako wa mtumiaji na kurasa nyingine
- Ukurasa wa mwongozo
- Jamii:Msaada (makala zilizomo humo zinaweza kusaidia mara nyingi)
- Ukurasa wa jumuia (pamoja na Wikipedia:Wakabidhi, penye majina walio tayari kukusaidia)
- Makala za msingi za Wikipedia
Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.
Ujue miiko:
- usilete kamwe matini wala picha kutoka tovuti za nje.
- usiingize matangazo ya kibiashara (pamoja na kuelekeza kwa kurasa zenye matangazo).
- usimwage kamwe matini kutoka google-translate au programu za kutafsiri.
- usitumie kama vyanzo vya taarifa au tanbihi <ref>Wikipedia (au mradi mwingine wa Wikimedia)</ref>, ila unaweza kutumia vyanzo vyake kwa kuvitaja vyenyewe moja kwa moja.
Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!
Welcome to Kiswahili Wikipedia!
We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:
- do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
- nor copied texts/images from other webs to this site!
- do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.
- do not use as references <ref>Wikipedia (or another project of Wikimedia)</ref>, though you can use their references by writing them themselves.
As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.
Madai bila thibitisho
[hariri chanzo]Simon salaam. Asante kwa kuchangia makala kwa Wikipedia hii. Lakini nakuomba kutokuandika madai ya uwezo wa matunda kutibu magonjwa bila kuonyesha marejeo. Mara nyingi unaweza kupata marejeo haya kwa Wikipedia ya Kiingereza. Asante. ChriKo (majadiliano) 17:52, 18 Septemba 2017 (UTC)
Sherehe!!!
[hariri chanzo]Angalia hatua aliyoifikisha Ndugu Riccardo: Matukio ya hivi karibuni. Sherehe!!! --Baba Tabita (majadiliano) 10:10, 17 Machi 2018 (UTC)
Utafiti
[hariri chanzo]Ndugu unaona nimesahihisha makala yako kuhusu milima ya Taurus. Naomba ukiendelea kutunga makala ujitahidi kufanya utafiti kwanza
- je makala gani zipo tayari (hivyo utumie majina yaleyale, na ingiza viungo kwao)
- chungulia chaguo cha maneno, tumia kamusi! (hivyo usijaribu kutafsiri mwenyewe maneno ya Kiingereza, mfano ulijaribu kutafsiri "mountain chain" kuwa mnyororo wa milima; lakini Kiswahili tunatumia "safu ya milima).
- usisahau kupanga makala katika jamii! (nimeiweka katika Jamii:Jiografia ya Uturuki)
Nimefurahi kuona juhudi yako, endelea lakini usisahau kuongeza umakini. Ukiwa n swali, uliza tu. Kipala (majadiliano) 18:26, 6 Agosti 2018 (UTC)
Vyanzo!!
[hariri chanzo]Hu uni ujumbe kwa watumiaji wetu TORY66, Elisha the great, Simon waziri msika na ALLY ROCKSTAR 4000. Naona ya kwamba mnaleta makala kuhusu wachezaji wa mpira. Napenda kuwapongeza kwa kazi hii! Ni muhimu pia nina uhakika ya kwamba wasomaji wengi watafurahi kupata habari zao kwa lugha yetu ya Kiswahili. Lakini kuna kasoro 3 katika makala zenu:
1. Wakati mwingine mnasahau Jamii au hamweki jamii zote. Hasa mnasahau kutaja jamii ya nchi. Chini ya kila makala ziwepo jamii. Mfano: [[Jamii: Mbegu za wachezaji mpira]] na [[Jamii:Wachezaji wa mpira wa (NCHI)]]
2. hakuna interwiki (yaani kiungo kwa makala juu ya mtu yeye yule katika lugha nyingine). Fanya hivi: baada ya kumaliza makala na kuipakua utaona chini upane wa kushoto maneno Add links. Bofya hapo utaona madirisha 2; juu andika en na kuthebitisha English (enwiki). Dirisha la chini andika lemma (yaani jina la makala), thibitisha, tayari. Kuanzia sasa makala yako itaonekana kwa kila wikipedia kwa lugha yoyote.
3. hakuna vyanzo. Maana yake hakuna uthebitisho kama huyu mtu yuko kweli au kama habari mnazoleta zina uthebitisho wowote. Zamani hatujajali sana lakini sasa imekuwa muhimu zaidi maana Wikipedia yetu ya Kiswahili imepata wasomaji wengi kiasi. Una njia mbili Kwanza tunga kila makala pamoja na vichwa vya
==Tanbihi==
<references/>
na
==Marejeo ya Nje==
„Tanbihi“ ni nafasi ya tanbihi (footnotes) na alama ya <references/> itaonyesha hapahapa footnotes ulizoweka katika matini.
Marejeo ya Nje ni nafasi kutaja tovuti, kitabu na kadhalika.
Kama makala ya Kiingereza ina sehemu ya "External links" basi bofya edit source, nakili yote na uiweke chini ya makala ya Kiswahili, chini ya kichwa "Marejeo ya Nje" .
Angalia habari juu ya mhusika ndani ya makala ya Kiingereza. Je kuna tanbihi? Kama ziko, bofya edit source (kuna fomati nyingine ambazo hatuwezi kuhamisha kwetu). Angalia kama reference inaanza na alama <ref>. Kama ni hivyo nakili reference yote kuanzia <ref> hadi alama ya <ref/> na ingiza mahali pake kwenye matini baada ya habari inayothibitishwa kwa chanzo hiki.
Angalia mfano wa makala Phil Jagielka nilipoongeza tanbihi na viungo vya nje. Naomba A) msisahau kuanzia sasa kuongeza sehemu hizi! na B) pia naomba mrudie makala mlizoweka tayari na kuboresha makala.
Mkiwa na swali mwulize Riccardo au mimi. Kipala (majadiliano) 19:03, 27 Agosti 2018 (UTC)
Document your culture with Wiki Loves Love 2019 and win exciting prizes!
[hariri chanzo]Please help translate to your language
Africa has many beautiful festivals, ceremonies and celebrations of love and we need your help to document these! They are the core part of African culture and in order to make sure this way of life followed by our ancestors remain among us, we need to have them online to make sure they are preserved. Join hands with Wiki Loves Love that aims to document and spread how love is expressed in all cultures via different rituals, celebrations and festivals and have a chance to win exciting prizes!! While uploading, please add your country code in the Wikimedia Commons upload wizard. If you want to organize an on-site Wiki Loves Love event, then contact our international team! For more information, check out our project page on Wikimedia Commons.
There are several prizes to grab. Hope to see you spreading love this February with Wiki Loves Love!
Imagine...The sum of all love!
Wiki Loves Love team 07:34, 4 Februari 2019 (UTC)
Vyanzo!! , Interwiki
[hariri chanzo]Mpendwa naona unaendelea kuanzisha makala bila kutaja vyanzo. Tafadhali urekebishe haraka. Usipojua jinsi gani, uniulize. Menginevyo soma Wikipedia:Mwongozo (Kutaja vyanzo)! Kipala (majadiliano) 07:06, 18 Novemba 2019 (UTC)
Kubadilisha jina la mtumiaji
[hariri chanzo]Asante, nimeona ombi lako. Sina madaraka maana mimi si steward. Peleka ombi lako hapa: https://meta.wikimedia.org/wiki/Special:GlobalRenameRequest na fuata maelezo. Kipala (majadiliano) 18:39, 9 Februari 2020 (UTC)
Tangazo
[hariri chanzo]Habari ndugu Mwanawikipedia!
Mimi ni mwezeshaji wa mradi uitwao Mwongozo Wa Kimataifa Wa Mwenendo Na Maadili. Ni mradi mchanga/mpya ambao Shirika la Wikimedia Foundation linanuia kuuanzisha endapo wadau wataona ni mradi unaofaa. Nakukaribisha usome mwongozo huo na kisha utoe maoni yako kwa kujibu maswali yote au baadhi yake kwa yale utakayopenda kuyatolea maoni HAPA
Taarifa zaidi kuhusu Mwongozo wa Kimataifa wa Nidhamu na Mwenendo
Shirika la Wikimedia Foundation lina mpango wa kuanzisha Mwongozo Wa Kimataifa Wa Mwenendo Na Maadili. Lengo la mwongozo huo ni kujaribu kuainisha vitu vya msingi vinavyopatikana katika miongozo midogo midogo iliyopo tayari katika kila jamii husika (mfano Jumuiya yetu hii ya wahariri wa Wikipedia ya Kiswahili). Lengo hasa la mwongozo huu ni kutengeneza mazingira ambayo wanawikipedia wote duniani watakuwa na uelewa wa pamoja juu ya vitu vya msingi kuhusu nini kinakubalika na kipi hakikubaliki wakati wa uchangiaji (uhariri) wa Wikipedia na pale wanawikipedia wanapowasiliana kwenye Wikipedia au ana kwa ana katika warsha na mikutano ya Wanawikipedia. Wazo hilo limekuja baada kukithiri kwa baadhi ya Wanawikimedia kukumbana kufanyiwa unyanyasaji wa kitabia (mfano matusi, kuitana majina yasiyofaa, kutishiana n.k) na Wanawikimedia wenzao, hivyo kuwakatisha tamaa ya kuendelea kuchangia katika miradi ya Wikimedia.Hivyo, wewe kama mdau muhimu katika miradi ya Wikimedia Foundation, unakaribishwa ku soma zaidi kuhusu mwongozo huo Hapana baada ya kuusoma mwongozo huo unaweza ku toa maoni yako Hapa kabla ya tar 15 April 2020.
Mwaliko wa kujiunga na kundi la Wahariri wa Wikipedia
Nakukaribisha ujiunge na kundi la Wahariri wa Wikipedia kutoka Dar es Salaam ili tuweze kujadiliana na kubadilishana uzoefu na mambo kadha wa kadha kuhusu Uhariri wa Wikipedia. Iwapo utapenda kujiunga, usisite kuwasiliana nasi kupitia wikitzagroup@gmail.com, na kwa taarifa zaidi kuhusu kundi la Wahariri wa Wikipedia wa hapa Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla na miradi waliyoitekeleza tayari, unaweza tembelea hapa ukurasa wao wa meta uitwao Wikimedia Community User Group Tanzania au pia katika Facebook kwa jila la Wikimedia Tanzania.
Ndimi AMtavangu (WMF) (majadiliano) 19:49, 5 Aprili 2020 (UTC)