Mahamadou Issoufou

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mahamadou Issoufou (amezaliwa 1 Januari 1951) ni mwanasiasa wa Niger ambaye amekuwa Rais wa Niger tangu tarehe 7 Aprili 2011.

Issoufou alikuwa Waziri Mkuu wa Niger kutoka mwaka 1993 hadi 1994, Rais wa Bunge la Kitaifa kuanzia mwaka 1995 hadi 1996, na alikuwa mgombea katika kila uchaguzi wa rais tangu 1993.

Aliongoza Chama cha Niger cha Demokrasia na Kijamaa (PNDS-Tarayya), chama cha kidemokrasia, tangu msingi wake 1990 hadi kuchaguliwa kwake kama Rais wa Niger mnamo 2011.

Wakati wa Urais wa Mamadou Tandja (1999-2010), Issoufou alikuwa kiongozi mkuu wa upinzaji.

Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mahamadou Issoufou kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.