Maendeleo ya Jamii
Maendeleo ya Jamii kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa hutafsiriwa kama Mchakato wa wanajamii kukusanyika pamoja kwa ajili ya kupata suluhisho la matatizo yanayowakabili [1].
Maendeleo ya jamii ni dhana pana inayotumika kwa viongozi, wanajamii, wanaharakati, ikiwahusisha wataalamu ili kuboresha maisha ya wanajamii pamoja na kutengeneza jamii iliyo bora.
Maendeleo ya jamii huelezewa kama fani ya kitaalamu na hufafanuliwa zaidi na jumuia za kimataifa kama Taaluma inayokuza demokrasia shirikishi, Maendeleo endelevu, haki, nafasi za kiuchumi, usawa, kuiwezesha jamii kimaslahi, kutambua hali za kimaisha na elimu.[2]
Maendeleo ya jamii husaidia kuwawezesha mtu mmojammoja na vikundi vya kijamii wenye mahitaji ya kuleta mabadiliko katika jamii zao. Maarifa hayo mara nyingi hufanyika kwa watu kupewa ujuzi na kuunda vikundi vitakavyokuwa na kazi na ajenda maalumu. Maafisa maendeleo ni lazima waelewe namna gani ya kufanya kazi zitakazoleta mabadiliko kulingana na asasi tofautitofauti.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Community development". UNTERM. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 14 Julai 2014. Iliwekwa mnamo 7 Julai 2014.
{{cite web}}
: More than one of|accessdate=
na|access-date=
specified (help); More than one of|archivedate=
na|archive-date=
specified (help); More than one of|archiveurl=
na|archive-url=
specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Alison Gilchrist; Marilyn Taylor (2011). The Short Guide to Community Development. Policy Press. ku. 2+. ISBN 978-1-84742-689-5.
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |