Macky Sall
Macky Sall (amezaliwa 11 Desemba 1961) ni mwanasiasa wa Senegal ambaye alikuwa Rais wa Senegal tangu tarehe 2 Aprili 2012 hadi 2 Aprili 2024, kisha kuchaguliwa tena mnamo Februari 2019. Yeye ndiye Rais wa kwanza kuzaliwa baada ya Senegal kupata uhuru kutoka Ufaransa.
Chini ya Rais Abdoulaye Wade, Sall alikuwa Waziri Mkuu wa Senegal kutoka Julai 2004 hadi Juni 2007 na Rais wa Bunge la Kitaifa kuanzia Juni 2007 hadi Novemba 2008. Alikuwa Meya wa Fatick kutoka mwaka 2002 hadi 2008 akashika wadhifa huo tena kutoka mwaka 2009 hadi 2012.
Sall alikuwa mwanachama wa muda mrefu wa Senegalese Democratic Party (PDS). Baada ya kugongana na Wade, aliondolewa kutoka wadhifa wake kama Rais wa Bunge la Kitaifa mnamo Novemba 2008; hivyo alijiunga na upinzaji akaanzisha chama chake mwenyewe kilichoitwa APR. Kuweka nafasi ya pili katika raundi ya kwanza ya uchaguzi wa rais wa 2012, alishinda msaada wa wagombea wengine wa upinzaji akamshinda Wade katika raundi ya pili ya kupiga kura, iliyofanyika tarehe 25 Machi 2012.
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Macky Sall kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |