Eurasia : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 1: Mstari 1:
[[Image:LocationEurasia.png|right|200px|thumbnail|Eneo la Eurasia]]
[[Image:LocationEurasia.png|right|200px|thumbnail|Eneo la Eurasia]]
[[Picha:Possible definitions of the boundary between Europe and Asia.png|300px|thumbnail|Njia mbalimbali za kuchora mpaka kati ya Ulaya na Asia]]
[[Picha:Boundary between Europe and Asia (green shade).png|300px|thumbnail|Njia mbalimbali za kuchora mpaka kati ya Ulaya na Asia]]
'''Eurasia''' ni jina la kutaja nchi zote za [[Asia]] na [[Ulaya]] kwa pamoja. Jina hili linaunganisha maneno "Europa" na "Asia".
'''Eurasia''' ni jina la kutaja nchi zote za [[Asia]] na [[Ulaya]] kwa pamoja. Jina hili linaunganisha maneno "Europa" na "Asia".



Pitio la 16:50, 15 Februari 2017

Eneo la Eurasia
Njia mbalimbali za kuchora mpaka kati ya Ulaya na Asia

Eurasia ni jina la kutaja nchi zote za Asia na Ulaya kwa pamoja. Jina hili linaunganisha maneno "Europa" na "Asia".

Hali halisi Ulaya na Asia ziko pamoja kama nchi kavu mfululizo na hakuna bahari inayoyatenganisha. Kwa hiyo Ulaya na Asia haziitwa mabara kwa sababu za kijiografia lakini kwa sababu za kihistoria na kiutamaduni tu. Uzoefu huu unatokana na Wagiriki wa Kale waliokuwa watu wa kwanza wa kugawa dunia katika sehemu tatu tofauti (Ulaya, Asia na Afrika) na hivyo kuweka msingi kwa ugawaji wa dunia kwa mabara.

Wataalamu wengi wa jiografia wanaana ya kwamba masi ya nchi kavu inayojumlisha Ulaya na Asia ina tabia zote za bara moja na hivyo hutumia jina la "Eurasia". Karibu eneo lote liko juu ya bamba la gandunia lilelile yaani Bamba la Ulaya-Asia.

Tangu kale swali la mpaka kati ya Ulaya na Asia lilikuwa tata na kuna majibu mbalimbali. Wengu hukubaliana ya kwamba msatri unafuata milangobahari ya Dardaneli na Bosporus (nchini Uturuki), mwambao wa Bahari Nyeusi na Bahari Kaspi halafu safu ya milima ya Ural hadi Bahari Aktiki. lakini kati ya bahari Nyeusi na kaspi katika eneo la Kaukasus mawazo hutofautiana sehemu gani ni ya Asia na zipi ya Ulaya.