Maulid : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d r2.7.2) (roboti Badiliko: kk:Мәулет мейрамы
d r2.7.1) (Roboti: Imeongeza fa:میلاد پیامبر
Mstari 45: Mstari 45:
[[en:Mawlid]]
[[en:Mawlid]]
[[es:Mawlid]]
[[es:Mawlid]]
[[fa:میلاد پیامبر]]
[[fr:Mawlid]]
[[fr:Mawlid]]
[[id:Maulid Nabi Muhammad]]
[[id:Maulid Nabi Muhammad]]

Pitio la 11:08, 6 Mei 2012

Maulid (pia: maulidi), Maulid an-Nabii ni sikukuu ya dini ya Uislamu ya kuzaliwa kwake Mtume Muhammad.

Neneo lenyewe ni la asili ya kiarabu kutokana na مولد النبي (maulid an-nabi) au (milaad an-nabi) ميلاد النبي . Sikukuu inafuata kalenda ya Kiislamu. Waislamu wa dhehebu la Sunni husheherekea tar. 12 Rabi'-ul-Awwal na Waislamu wa dhehebu la Shia husheherekea tarehe 17. Rabi'-ul-Awwal. Muhammad alizaliwa takriban mwaka 570 BK.

Wataalamu wa historia wengine wanasema ya kwamba sherehe ya Maulid imeanzishwa mnamo karne ya 12 BK. Kuna Waislamu kadhaa wanaokataa sherehe hiyo kwa sababu hakuna sunna wala hadith ya Muhammad mwenyewe kuhusu kusheherekea maulid yake. Lakini kwa ujumla ni sikukuu inayopendwa sana na Waislamu wengi duniani.

Kati ya desturi ni mikutano, kusikia mashairi juu ya maisha ya mtume a mengine. Misri maulid ni kati ya sikukuu za kiislamu zinazokumbukwa sana na Waislamu. Katika Afrika ya Mashariki sherehe ya maulid huko Lamu imejulikana hasa ikivuta wageni kutoka pande zote za Afrika ya Mashariki hadi Uarabuni.

Tarehe za Maulid katika kalenda ya Gregori

Maulid kama vile sikukuu zote za Kiislamu inafuata kalenda ya Kiislamu ambayo ni kalenda ya mwezi. Kwa sababu hiyo tarehe yake hubadilika katika kalenda ya Gregori au kimataifa.

Zifuatazo ni tarehe za maulid kwa ajili ya miaka 2006 - 2021. Tarehe ya kwanza ni ile ya Wasunni (12 Rabi'-ul-Awwal) na tarehe ya pili katika mabano ni ile ya Washia (17. Rabi'-ul-Awwal). Tarehe hizo zinaweza kuwa tofauti na tarehe halisi kwa sababu kuna tofauti kati ya nchi na vikundi vya Waislamu jinsi gani kukubali kuhusu mwanzo wa miezi.

  • 2006: Aprili 12, (Aprili 17)
  • 2007: Machi 31, (Aprili 5)
  • 2008: Machi 20, (Machi 25)
  • 2009: Machi 9, (Machi 14)
  • 2010: Februari 26, (Machi 3)
  • 2011: Februari 15, (Februari 20)
  • 2012: Februari 4, (Februari 9)
  • 2013: Januari 24, (Januari 29)
  • 2014: Januari 13, (Januari 18)
  • 2015: Januari 2, (Januari 7)
  • 2016: Disemba 22, (Disemba 27)
  • 2017: Disemba 11, (Disemba 16)
  • 2018: Novemba 30, (Disemba 5)
  • 2019: Novemba 19, (Novemba 24)
  • 2020: Novemba 8, (Novemba 13)
  • 2021: October 28, (Novemba 2)

Viungo vya nje