Meli : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
New page: thumb|Jahazi '''Meli''' ni chombo kikubwa cha usafiri kwenye maji. Siku hizi meli huwa na bodi ya chuma ikisogezwa kwa nguvu ya injini inayochoma [[diseli...
 
No edit summary
Mstari 29: Mstari 29:
Katika karne ya 19 injini ya mvuke ilipatikana hata kwa meli. Meli zikawa kubwa zikaendlea kukua wakati injini za diseli zimepatikana katika karne ya 20.
Katika karne ya 19 injini ya mvuke ilipatikana hata kwa meli. Meli zikawa kubwa zikaendlea kukua wakati injini za diseli zimepatikana katika karne ya 20.


[[Image:Supertanker AbQaiq.jpg|thumb|300px|Meli kubwa ya mizigo ya kubeba mafuta ya petroli]]
[[Image:Supertanker AbQaiq.jpg|thumb|300px|Meli kubwa ya shehena ya mafuta ya petroli]]


[[Category:Meli| ]]
[[Category:Meli| ]]

Pitio la 14:48, 8 Septemba 2008

Jahazi

Meli ni chombo kikubwa cha usafiri kwenye maji. Siku hizi meli huwa na bodi ya chuma ikisogezwa kwa nguvu ya injini inayochoma diseli. Hadi karne ya 19 meli zilijengwa kwa kutumia ubao zikasongezwa hasa kwa nguvu ya upepo kwa kutumia tanga. Jahazi ziko hadi leo.

Meli hutumiwa hasa kwa kubeba mizigo na abiria. Kuna pia meli za kijeshi zinazoitwa manowari.

Muundo wa meli ya kisasa

Muundo wa meli

  1. Omo ni sehemu ya mbele ya bodi ya meli
  2. Pua la omo linapunguza ukinzani wa maji wakati wa mwendo na kupunguza matumizi ya mafuta ya injini
  3. Nanga hushukwa hadi ya chini na kushika meli ikisimama
  4. Bodi ya meli imetengenezwa kwa mabamba ya feleji
  5. Rafadha (au: jembe) ya meli inasogeza chombo mbele ndani ya maji
  6. Tezi (au: shetri) ni sehemu ya nyuma ya meli
  7. Dohani ni faneli au eksosti kwa hewa chafu ya injini
  8. Majengo juu ya sitaha ni kama nyumba kwa ajili ya mabaharia na abiria, huwa pia na chumba cha kutawala meli
  9. Sitaha ni uso wa juu wa meli; ni dari juu ya bodi ya meli; meli kubwa huwa na sitaha mbalimbali chini ya sitaha ya juu


Historia

Vyombo vya usafiri vya kwanza kwenye maji yalikuwa mashua na maboti madogo kama mtumbwi.

Kuanzia mwaka 4000 KK watu wa Misri ya Kale wameanza kutengeneza jahazi ndogo. Manmo 1200 KK watu wa Finisia na Ugiriki ya Kale walijenga jahazi kubwa zaidi yenye urefu wa mita 30. Wachina wanajulikana walijenga jahazi kuanzia 2000 KK. Waroma wa Kale walitengeneza meli iliyobeba watu 1,000.

Katika mazingira ya Mediteranea meli hizi za kwanza zilisogezwa kwa kasia pamoja na tanga. Meli kubwa za kiroma zilikuwa na kasia kubwa zilizopigwa na watumwa wawili au watatu kwa kila kasia.

Jahazi ziliboreshwa hadi kuvuka bahari kuanzia karne ya 15 BK. Wachina na Wareno ni watu wa kwanza waliovuka bahari za mbali. Ila tu Wachina baada ya kutembelea mara kadhaa pwani za Afrika chini ya Zheng He mnamo mwaka 1400 waliamua kuacha upelelezi huu lakini Wareno waliendelea kuvuka Afrika na dunia yote na kuanzisha kipindi cha ukoloni cha Ulaya.

Katika karne ya 19 injini ya mvuke ilipatikana hata kwa meli. Meli zikawa kubwa zikaendlea kukua wakati injini za diseli zimepatikana katika karne ya 20.

Meli kubwa ya shehena ya mafuta ya petroli