Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d robot Modifying: eu:Lehen Mundu Gerra
Mstari 73: Mstari 73:
[[it:Prima guerra mondiale]]
[[it:Prima guerra mondiale]]
[[ja:第一次世界大戦]]
[[ja:第一次世界大戦]]
[[ka:პირველი მსოფლიო ომი]]
[[ko:제1차 세계 대전]]
[[ko:제1차 세계 대전]]
[[la:Bellum Orbis Terrarum I]]
[[la:Bellum Orbis Terrarum I]]

Pitio la 09:07, 8 Agosti 2006

Shirikiano za kijeshi katika Ulaya wakati wa mwaka 1915. Nyekundu: Mataifa ya Kati; kijani: Mataifa ya Ushirikiano; njano: mataifa yasiyoshiriki vitani
Ramani ya dunia ikionyesha nchi na maeneo yaliyoshiriki katika Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Kijani: Mataifa ya Ushirikiano; njano: Mataifa ya Kati; nchi zisizoshiriki kwa rangi ya kijivu

Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia ilikuwa vita kati ya 1914 hadi 1918 ya Ujerumani, Austria-Hungaria, Bulgaria na Uturuki (ziliitwa "Mataifa ya Kati") dhidi ya Ufaransa, Urusi, Uingereza, Marekani na nchi mbalimbali zilizoshirikiana nazo (zilitwa "Mataifa ya Ushirikiano").

Vita hii ilianza katika Ulaya ikapanuka haraka hadi Mashariki ya Kati, Afrika na Asia ya Mashariki ikasababisha kifo cha takriban watu milioni tisa.

Sababu na matokeo

Sababu yake ilikuwa mashindano makali kati ya mataifa ya Ulaya kuhusu kipaumbele duniani.

Matokeo yake yalikuwa mwisho wa kipaumbele cha Ulaya duniani na kupanda ngazi wa Marekani, mapinduzi katika nchi mbalimbali, mwisho wa falme za Ujerumani, Austria na Urusi pamoja na mwanzo wa utawala wa kikomunisti katika Urusi, mwisho wa Dola la Austria - Hungaria na Dola la Uturuki ya Kiosmani pamoja na mwisho wa ukoloni wa Kijerumani duaniani.

Katika Ulaya nchi mpya zilijitokeza kama vile Czechoslovakia, Finland, Latvia, Lithuania, Estonia na Yugoslavia pamoja nchi zilizorudi katika uwanja wa kimataifa ndizo Austria, Hungaria na Poland.

Mwanzo wa vita

Vita ilianza kutokana na ugomvi kati ya Austria-Hungaria na Serbia. Kutokana na muundo wa mikataba ya usaidizi kati ya nchi za Ulaya mwanzo huo ulisababisha nyororo ya matangazo ya hali ya vita kati ya mataifa mengine.

Tar. 28. 06. 1914 katika mji wa Sarayevo mwana wa Kaisari wa Austria aliyekuwa mfalme-teule akauawa pamoja na mke wake na mgaidi Mserbia mwanachama wa kundi la "Mkono Mweusi" lililosikitika utawala wa Austria-Hungaria katika Bosnia. Austria ilidai Serbia ifuate mashariti makali katika utafiti wa tendo lile. Serbia ilipokataa sehemu ya masharti Austria ilitangaza hali ya vita dhidi ya Serbia tar. 28.07.1914.

Agosti ya 1914 iliona kupanuka kwa vita hii: Warusi walikuwa na mkataba wa usaidizi na Serbia wakatangaza hali ya vita dhidi ya Austria-Hungaria. Sasa wakaingia Wajerumani waliokuwa na mapatano ya Usaidizi na Austria-Hungaria wakitangaza hali ya vita dhidi ya Urusi. Urusi kwa upande wake ulikuwa na mkataba wa kusaidiana na Ufaransa hivyo hali ya vita ikajitokeza pia kati ya Ufaransa na Ujerumani. Uingereza ulijiunga na vita baada ya Wajerumani walipoanza kuingia ndani ya eneo la Ubelgiji kwa shabaha ya kuvuka haraka ili wavamie kaskazini ya Ufaransa.

Kuanzia Oktoba 1914 Dola la Uturuki lilijiunga na vita kufuatana na mkataba wake wa siri na Ujerumani. Mwaka 1915 Italia ilijiunga na Wafaransa na Waingereza kwa kushambulia Austria-Hungaria.

Vita katika nchi mbalimbali

Vita ilipigwa kwa ukali miaka iliyofuata. Wajerumani waliingia ndani ya Ufaransa lakini walikwama kabla ya kufika mji mkuu wa Paris. Kwa muda mrefu mstari wa mapambano ulibaki palepale. Katika Mashariki Wajerumani walifauli kurudisha mashambulio ya kirusi na kuteka sehemu za Urusi. Katika Kusini ya Ulaya Waustria walifaulu kwa matatizo makubwa kuteka Serbia na Montenegro pamoja na Albania. Waturuki walishindwa kwa ujumla katika mashambulio yao dhidi ya Warusi katika eneo la Kaukasus na dhidi ya Waingereza katika Misri. Lakini walifaulu kuwarudisha mashambulio ya Kiingereza dhidi ya Uturuki mwenyewe. Waingereza walifaulu pia katika Irak kuwarudisha Waturuki.

Vita katika koloni

Vita ilienea haraka baharini na katika koloni za nchi za Wajerumani zilizovamiwa na Waingereza, Wafaransa, Afrika Kusini na Japani. Kwa ujumla koloni zote zilitekwa haraka isipokuwa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani. Jeshi la Ulinzi wa Kijerumani chini ya uongozi wa Paul von Lettow-Vorbeck ilifaulu kupigania jeshi kubwa sana wa Waingereza bila kumalizwa hadi Novemba 1918.

Mwisho wa vita

Wakati wa 1917 mataifa ya Ulaya yalionyesha dalili za uchovu. Katika hali hii mabadiliko mawili makubwa yalitokea: Marekani ilijiunga na vita dhidi ya Wajerumani na Urusi uliona mapinduzi iliyolazimisha serikalimpya kutia sahihi mapatano ya kumaliza mapigano dhidi ya Wajerumani walioteka maeneo makubwa katika Urusi.

Nguvu ya Marekani ilionekana haraka na bahati ya Ujerumani ilipungua sana. Austria-Hungaria ilidhoofishwa vilevile.

Mwaka 1918 iliona mwisho wa vita. Madola ya Austria na Uturuki yalikwisha na sehemu zao zilikuwa nchi mpya au nchi zilizoundwa upya.

Mkataba wa Versailles

Mkutano wa Versailles uliamua masharti makali dhidi ya Ujerumani katika Mkataba wa Versailles. Koloni za Ujerumani zilikabidhiwa na Shirikisho la Mataifa kama maeneo ya kukabidhiwa kwa Uingereza, Ufaransa, Ubelgiji, Japani, Afrika Kusini na Australia.

Versailles ilikuwa jaribio la kuunda utaratibu mpya duniani uliotakiwa kulindwa na Shirikisho la Mataifa. Lakini ukosefu wa nguvu kwa upande wa Shirikisho la Mataifa pamoja na kuanza na kupanuka kwa mwendo mpya wa kifashisti iliyochukua utawala katika Italia na Ujerumani ulishinda nia hiyo. Wataalamu wasio wachache wanasema ya kwamba mwisho wa vita kuu ya kwanza ulipanda tayari mbegu wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia.