Lydie Dooh Bunya
Mandhari
Lydie Dooh Bunya (anajulikana pia kwa jina lake la ndoa kama Quan-Samé; alizaliwa Douala, Kamerun, 1933) ni mhariri anayefanyia kazi huko Paris, mwandishi na pia ni mpiganaji wa haki za wanawake.[1]
Maisha yake
[hariri | hariri chanzo]Lydie Sophie Dooh Ebenye Bunya, baba yake alikuwa afisa wa forodha na mama yake alikuwa fundi wa kushona nguo. Baada ya kuanza masomo yake huko Kamerun, Dooh Bunya alihitimu masomo yake ya sekondari huko nchini Ufaransa, kwenye shule ya wasichana huko Saint-Gaultier. Akiwa kama mwanachuo huko, alianza kwa kusomea unesi na kemia kabla ya kujikita na shahada ya fasihi.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Lydie Dooh Bunya (uwa.edu.au)