Nenda kwa yaliyomo

Luciano wa Samosata

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Luciano jinsi mchoraji wa karne ya 17 alivyomwaza.

Luciano wa Samosata (takriban 125 – baada ya 180) alikuwa mhutubu na mwandishi kutoka mji wa Samosata katika Syria wakati wa Dola la Roma. Lugha yake ya asili pengine ilikuwa Kisirya lakini kazi zake zote zilizohifadhiwa zimeandikwa kabisa kwa Kigiriki cha Kale. Mtindo wa maandiko yake ulikuwa hasa tashtiti ambamo alikejeli ushirikina na desturi za kidini.

Luciano alikuwa na athari kubwa katika fasihi ya Magharibi. Kazi zilizochochewa na maandishi yake ni pamoja na Utopia ya Thomas More, kazi za François Rabelais, Timon of Athens ya William Shakespeare na Safari za Gulliver ya Jonathan Swift.

Zaidi ya kazi 80 zinazoaminiwa kuandikwa na Luciano zimehifadhiwa. Luciano alilenga hadhira ya Kigiriki iliyoelimika sana, ya tabaka la juu.

Lucian alikuwa mmoja wa waandishi wa kwanza wa riwaya katika ustaarabu wa magharibi. Hadithi ya Kweli ( Ἀληθῆ διηγήματα ) ilikuwa kazi ya masimulizi ya kubuni. Katika hadithi hii aliiga baadhi ya hadithi za ajabu zilizosimuliwa na Homer katika Odisei na pia habari zilizorekodiwa na mwanahistoria Thucydides . [1] [2] Alitarajia mandhari ya kisasa bunilizi ya kisayansi ikiwa ni pamoja na safari za kwenda mwezini na hadi Zuhura, uhai wa nje na vita kati ya sayari. Riwaya hiyo mara nyingi huchukuliwa kuwa kazi ya kwanza inayojulikana ya bunilizi ya kisayansi. [3] [4] [5]

  • The Works of Lucian from the Greek. Juz. la I. Ilitafsiriwa na Francklin, Thomas. London: T Cadell. 1780 – kutoka Google Books.; volume II; volume III; volume IV.
  • Lucian of Samosata from the Greek with the Comments and Illustrations of WIELAND and Others. Juz. la I. Ilitafsiriwa na Tooke, William. London: Longman, Hurst, Rees, Orme, and Brown. 1820. Iliwekwa mnamo 22 Januari 2021 – kutoka Internet Archive.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link); volume II.
  • Lucian’s True History, with illustrations by Aubrey Beardsley, William Strang, and J. B. Clark, privately printed in an edition of 251 copies, 1894.[6]
  • The Works of Lucian of Samosata. Complete with exceptions specified in the preface. Juz. la I. Ilitafsiriwa na Fowler, H. W.; Fowler, F. G. Oxford: Clarendon Press. 1905.; volume II; volume III; volume IV.
  • Lucian with an English translation (Loeb Classical Library), in 8 volumes: vols. 1–5 ed. Austin Morris Harmon (1913, 1915, 1921, 1925, 1936); vol. 6 ed. K. Kilburn (1959); vol. 7–8 ed. Matthew Donald Macleod (1961, 1967).
  • Neil Hopkinson (ed.), Lucian: A Selection. Cambridge Greek and Latin Texts (Cambridge/New York: Cambridge University Press, 2008).
  • Lightfoot, Jane (2003). On the Syrian Goddess. Oxford University Press. ISBN 978-0-19-925138-4.
  1. C. Robinson, Lucian and his Influence in Europe (London, 1979), 23–25.
  2. A. Bartley, 2003, "The Implications of the Reception of Thucydides within Lucian's 'Vera Historia'", Hermes Heft, 131, pp. 222–234.
  3. Grewell, Greg: "Colonizing the Universe: Science Fictions Then, Now, and in the (Imagined) Future", Rocky Mountain Review of Language and Literature, Vol. 55, No. 2 (2001), pp. 25–47 (30f.).
  4. Fredericks, S.C.: “Lucian's True History as SF”, Science Fiction Studies, Vol. 3, No. 1 (March 1976), pp. 49–60.
  5. Swanson, Roy Arthur: "The True, the False, and the Truly False: Lucian's Philosophical Science Fiction", Science Fiction Studies, Vol. 3, No. 3 (November 1976), pp. 227–239.
  6. “Beardsley (Aubrey Vincent)” in T. Bose, Paul Tiessen, eds., Bookman's Catalogue Vol. 1 A-L: The Norman Colbeck Collection (UBC Press, 1987), p. 41

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]