Lucas Digne

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Lucas Digne

Lucas Digne (matamshi ya Kifaransa: [lykɑ diɲ]; alizaliwa Julai, 1993) ni mchezaji wa soka wa Ufaransa anayecheza kama beki wa kushoto, katika klabu ya Uingereza, Everton na timu ya taifa ya Ufaransa.

Digne alianza kazi yake ya soka Lille kabla ya kujiunga na Paris Saint-Germain mwaka 2013. Baada ya kutumia msimu mmoja kwenda kwa mkopo huko Roma, alihamia Barcelona F.C. mwezi Julai 2016. Pamoja na kukosa kucheza mara kwa mara kwenye klabu yoyote, alishinda tuzo 12 huko Paris na Barcelona. Alijiunga na Everton mwezi Agosti 2018.

Alishinda Kombe la Dunia 2013 na Ufaransa chini ya miaka 20, na alifanya mechi yake ya kimataifa ya mwezi Machi, 2014. Aliwakilisha Ufaransa katika Kombe la Dunia la FIFA 2014 na UEFA Euro 2016, ambapo taifa lake lilifikia fainali.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Lucas Digne kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.