Luangwa (mto)
Mto Luangwa | |
---|---|
| |
Chanzo | Milima ya Mafinga, Zambia |
Mdomo | Mto Zambezi |
Nchi za beseni ya mto | Zambia, Malawi, Msumbiji |
Urefu | km 806 |
Kimo cha chanzo | m 1,500 |
Kiasi cha maji kinachotolewa mdomoni | m³/s 31.6 |
Eneo la beseni (km²) | km² 145,700 |
Mto Luangwa ni mto mkubwa wa Zambia ya mashariki.
Kuna mto wa pili mdogo zaidi wenye jina hilohilo unaoishia katika Ziwa Kariba.
Mwendo
[hariri | hariri chanzo]Luangwa ina chanzo chake katika milima ya Mafinga karibu na mpaka wa Tanzania na Malawi. Kwa jumla huelekea kusini sambamba na mpaka wa Malawi. Unapita maeneo mapana ya hifadhi za taifa za Luangwa Kaskazini na Luambe hadi Luangwa Kusini.
Takriban kilomita 500 baada ya chanzo bonde la mto linakuwa jembamba lenye magenge makali kila upande. Kabla ya mdomo wake mto Luangwa ni mpaka kati ya Zambia na Msumbiji.
Mto unaishia katika Zambezi kwenye mji wa Luangwa.
Mabadiliko makubwa ya kiwango cha maji
[hariri | hariri chanzo]Kiasi cha maji ndani ya mto hubadilika sana kufuatana na majira. Wakati wa ukame mto una maji kidogo na mahali pengi unapitika kwa miguu. Lakini kati ya Desemba hadi Machi wakati wa mvua katika milima ya chanzo chake na cha matawimto kuna maji mengi. Kila mwaka mwendo wa mto unaweza kubadilika kiasi kutokana na nguvu ya maji. Hii ni sababu mojawapo ya kwamba hakuna watu wengi wanaokaa kando ya mto huu.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Luangwa (mto) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |