Nenda kwa yaliyomo

Lomboko

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Lomboko ilikuwa kambi ya watumwa katika maeneo ya Sierra Leone ya leo. Ilikuwepo kwenye mdomo wa mto Gallinas katika Atlantiki.

Iliundwa na kudhibitiwa na mfanyabiashara maarufu wa watumwa, Pedro Blanco kutoka Hispania. [1] Ilikuwa na magereza kadhaa ya kushikilia watumwa walioletwa kutoka maeneo ya ndani, na pia majengo makubwa kadhaa ya Blanco kuwaweka wake zake, masuria, na wafanyakazi

Lomboko ilitawanyika katika visiwa vidogo kadhaa kwenye mdomo wa Mto Gallinas, karibu na Sulima kwenye pwani ya Gallinas. [2] Wafanyabiashara wa watumwa kutoka Hispania walidhibiti eneo hilo, ndani ya koloni la Kiingereza la Sierra Leone. Kufikia mwaka 1839, karibu watumwa 2,000 kwa mwaka walikuwa wakitoka kwenye Mto Gallinas, licha ya biashara ya watumwa kuwa haramu tangu mwaka 1818. Mnamo 1849, kikosi cha Jeshi la Wanamaji la Uingereza kilishambulia Lomboko. Watumwa waliachiliwa na kisha majengo ya Lomboko yaliangamizwa kabisa. [3]

Ngome hiyo ilipewa nafasi katika filamu Amistad ya Steven Spielberg inayosimulia historia ya uasi wa watumwa kwenye jahazi La Amistad. Katika filamu hiyo, mhusika mkuu Joseph Cinqué, pamoja na watumwa wengine, wanaonyeshwa wakikamatwa na kuletwa Lomboko na kutendewa kinyama. Ukombozi wa watumwa na uharibifu wa ngome hiyo vinaonyeshwa katika kilele cha filamu. [4]

  1. Lawrance, Benjamin Nicholas (2015). Amistad's Orphans: An Atlantic Story of Children, Slavery, and Smuggling. Yale University Press. uk. 118. ISBN 0-300-19845-0.
  2. Rediker, Marcus (2012). The Amistad Rebellion: An Atlantic Odyssey of Slavery and Freedom. Penguin. ISBN 1-101-60105-1.
  3. Grayson, Robert (2011). The Amistad. Edina, Minn.: ABDO Pub. uk. 7. ISBN 1-61714-761-3. royal navy lomboko 1849.
  4. Zafiris, Anna (2010). The Representation of African Americans in Steven Spielberg's 'Amistad'. München: GRIN Verlag. uk. 4. ISBN 3-640-52511-6.