Lobamba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Lobamba
Nchi Uswazi
mahali pa Lobamba nchini Uswazi

Lobamba ni moja kati ya miji mikuu miwili ya Uswazi. Lobamba ni mji mkuu wa mfalme na pia makao ya bunge la nchi. Serikali inakaa Mbabane.

Lobamba inaona sherehe kubwa ya kitaifa kila mwaka ni ngoma ya Umhlanga au ngoma ya mafunjo ambako wasichana wanachukua mafunjo na kuzipeleka kwa ikulu ya ntombi (mama wa mfalme). Ni kawaida ya kwamba mfalme anaweza kumteua mke mpya kati ya wasichana hawa wakicheza.

Majengo maalumu ni pamoja na ikulu, boma la kifalme, jumba la mama wa mfalme, Makumbusho wa Kitaifa ya Uswazi, Bunge na makumbusho kwa mfalme Sobhuza II wa Uswazi.